Wednesday, February 4, 2009

Wapiga Debe

Moja ya ajali mbaya za barabarani zilitokea Mkoani Mbeya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 15
Hapa Mbeya kwa takribani siku nne sasa kuanzia Januari 31, kuna shughuli pevu inaendelea dhidi ya wapiga debe na madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi.
Hadi kufikia jana wapiga debe zaidi ya 163 wamekamatwa , 143 walifikishwa mahakamani jana na kati ya hao 93 waliachiwa kwa dhamana na wengine 53 kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Lakini hali ikiwa hivyo leseni za madereva 85 wa daraja 'C' ambao wanaamini ni madereva bora kabisa zinashikiliwa na polisi na wanashughuli ya kujaribiwa upya kutokana na kuonekana kuwa ni madereva jeuri na wasiozingatia sheria za usalama barabarani hali inayomtia shaka RPC Zelothe Stephen.
Ndugu zangi hivi ni kweli abiria, wanahitaji kuelekezwa magari ya kupanda wakati hivi sasa mengi yana vibao vinavyoelekeza maeneo mbalimbali wanayotaka kwenda?
Nchi ikiwa imegubikwa na ajali za kutisha zinatokana na madereva wasiojali, Je madereva wanaosababisha ajali kwa makusudi, kwanini wasizuiwe kuendesha magari tena, tunasemaje kuhusu hilo?

No comments:

Post a Comment