Thursday, December 19, 2013

Elimu

Kukosa kuungwa mkono na wazazi, walezi pamoja na kuamini kuwa kunahitajika nguvu kubwa katika utendaji wa kazi imedaiwa kuwa chanzo cha wasichana kukimbia masomo ya sayansi na uhandisi.

Hayo yalisemwa na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya mafundi wa majokofu na viyoyozi kuhusu teknolojia mbadala za upozaji rafiki kwa tabaka la Ozoni yanayofanyika katika Hoteli ya Paradise Jijini Mbeya.

Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Must), Moses Malole alisema kuwa imani kuwa kazi za uhandisi zinahitaji matumizi ya nguvu pamoja na kutoungwa mkono na wazazi imekuwa ni kichochea cha idadi kubwa ya wasichana kuyaepuka masomo ya uhandisi na sayansi.

Wednesday, December 18, 2013

Kilimo

Wakulima wilayani Chunya wameingiza shilingi bilioni 90 katika msimu wa kilimo uliopita kutokana na mauzo ya mazao ya ufuta,karanga, alizeti na tumbaku.
Mkuu wa wilaya ya Chunya, Deodatus Kinawilo aliyasema hayo alipokuwa akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kuvijengea uwezo vikundi vya wakulima wa zao la alizeti wilayani humo.
Alisema kuwa kutokana na mapato hayo inadhihirisha kuwa shughuli za kilimo zinamanyfaa kiuchumi kutokana na wakulima kuweza kupata shilingi bilioni tisini katika msimu mmoja wa kilimo ambapo alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuacha kulalamikia ugumu wa maisha na badala yake wafanye kazi.
Akitoa mchanganuo wa mapato hayo, Kinawilo alisema wakulima wa alizeti walipata shilingi bilioni nne, ufuta bilioni 27, karanga bilioni 12 na tumbaku bilioni 47, hata hivyo alisema licha ya mapato hayo eneo linalolimwa ni dogo ikilinganishwa na eneo linalofaa kwa kilimo.

Wednesday, December 11, 2013

Michezo


 Hatimaye baada ya hadithi za muda mrefu na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuufungia uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mbeya, iwanja huo umeanza kufanyiwa ukarabati katika eneo la kuchezea (pitch) ili uweze kuwa kwenye kiwango na kuweza kutumika kwa michuano mbalimbali ya mpira wa miguu.

Meneja wa Uwanja huo, Modestus Mwaluka anasema tatizo la uwanja huo sio kubwa sana na ukarabati wake utakuwa ni wa muda mfupi na uwanja utakuwa tayari kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom.

 Picha ya juu na chini zikionyesha ukarabati unaoendelea katika uwanja huo ambao unatumiwa na timu ya Tanzania Prisons na Mbeya City kama uwanja wa nyumbani. Mara kadhaa uwanja huo umekuwa ukilalamikiwa hasa na timu za Yanga na Simba kuwa ni mbovu na haufai hasa katika nyakati ambazo zinashindwa kuibuka na ushindi na zikishinda uwanja huwa unakuwa ni mzuri.


Hata hivyo pamoja na ukarabati wa sehemu ya kuchezea bado wamiliki wa uwanja huo wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha uwanja huo unakuwa katika hali ya usafi na kuboresha mazingira katika nyakati zote ikiwemo kujenga vyoo vipya kwa ajili ya mashabiki wa soka na wananchi wanaofika uwanjani hapo kwa shughuli mbalimbali.

Thursday, December 5, 2013

Kweli tatizo la vijana sio siasa

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana amesema kuwa tatizo la vijana nchini si siasa na vyama vya siasa kama CCM, Chadema au NCCR Mageuzi na kwamba tatizo lao kubwa ni ukosefu wa ajira.

Kinana aliyasema hayo jana wakati akifuhutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini Mbeya ambapo alisema kuwa vijana wamekuwa wakijihusisha na maandano ya kisiasa wakiamini wanaweza wakapata chochote.

Alisema kuwa ili kuwawezesha vijana kujiajiri ipo haja kwa serikali kufufua viwanda vilivyokufa, hata hivyo alisema kuwa serikali haiwezi kuajiri watanzania wote bali inatakiwa kutengeneza mazingira yatakayowawezesha vijana kujiajiri.

Wednesday, December 4, 2013

Hatari kwa afya

Mtoto akichota maji machafu katika dimbwi la Maji, ni muhimu kwa wazazi kuwa makini kwa kuwaangalia watoto michezo wanayocheza na vitu wamavyochezea ili kuhakikisha wanakuwa na afya nje na hawapati magonjwa ya kuambukiza ambauo ni hatari kwa afya zao.

Thursday, November 28, 2013


Watoto wakisakata kabumbu huku wakiwa pekupeku na mpira wa makaratasi maarufu kama kinyenga, vipaji vingi vya watoto vimekuwa vikipotelea mtaani kutokana na kukosekana kwa mfumo bora wa kuendeleza vipaji vya watoto.

Wednesday, November 27, 2013

 Wafanyabiashara wa matikiti maji wakisubiria wateja wanaosafiri kutoka Dodoma ili wawauzie bidhaa zao na wao kupata fedha za kujikimu na kuendeleza biashara zao ndogo.

Mandhari ya milima ya kueleka Iringa kutokea Mtera, ni milima yenye mandhari ya kuvutia na ujenzi wa kiwango cha lami ukiwa unaendelea. Kuboreshwa kwa miundo mbinu ya barabara kunasaidia kuboresha na kurahisisha usafiri wa kutoka eneo moja kwenda lingine na hivyo kuharakisha shughuli za maendeleo

Tuesday, November 26, 2013

Wakinamama wafanyabiashara ndogo wakiwaonyesha bidhaa abiria (hawapo pichani) waliokuwa wakisafiri kati ya Dodoma, Mtera, Iringa na Mbeya, licha ya uchumi mdogo biashara ndogo zimekuwa zikiwawezesha wanawake kumudu kuhudumia familia na kusomesha watoto wao kwa mafanikio.

     Mandhari ya maeneo ya mtera, unaposafiri kutoka Dodoma kuelekea Mkoani Iringa au Mbeya, ipo haja ya kutunza mazingira ili kuendelea kuwa na maeneo ya kuvutia nchini.

Unaposafiri na basi ya Dodoma Mbeya kupitia Mtera abiria kujazana kupita kiasi huku wengine wakiwa wamebeba kuku ni jambo la kawaida kabisa, ipo haja kwa wataalamu wa afya kueleza athari za watu kujazana kupita kiasi katika vyombo vya usafiri huku wakiwa wamebeba mifugo
Dk. Mwakyembe kufungua maonyesho ya kimataifa ya biashara
 
Waziri wa uchukuzi, Dk. harrison Mwakyembo leo anatarajia kuzindua maonyesho ya kimataifa ya biashara yatakayofanyika kwa wiki moja katika viwanja vya ukumbi wa mikutano wa mkapa uliopo Jijini Mbeya.
 
Maonyesho hayo yanatarajia kushirikisha makampuni kutoka nje ya nchini yakiwemo kutoka nchini Kenya na makapuni ya ndani ya nchi ambapo hadi kufikia jana maandalizi yalikuwa yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 90 kwa washiriki kupanga bidhaa zao.

Sunday, November 24, 2013

Dodoma kupitia Mtera kwenda Mbeya

*Safari ya jasho, mateso na vilio kwa watoto.

Njia iliyozoeleka kwa wasafiri wanaotoka Mkoa wa Mbeya kwenda Makao Makuu ya nchi Mkoani Dodoma ni kupitia Mikoa Iringa, Morogoro na hatimaye Dodoma  ambapo safari ni takribani zaidi ya masaa 14 barabarani kwa maana unaondoka Mbeya saa 12 asubuhi na kufika      Dodoma kati ya saa 1 na saa 2 usiku.

Lakini ukapatikana ushauri kuwa unaporudi Mbeya, panda basi linalopita njia ya Makato kutoka Dodoma, Mtera, Iringa na Mbeya na kuwasili Mbeya majira ya saa 7 au 8 mchana

Friday, November 15, 2013

Eti Mwanafunzi wa chuo cha Ualimu uyole, aliyetajwa kwa jina moja la Joseph anadaiwa kukutwa akiwa amejinyonga katika mto nzovwe uliopo Jijini Mbeya.marehemu alikuwa anachukua degree mwaka wa kwanza, sababu ya kujinyonga haijajulikana, mwili wa marehemu upo rufaa

Thursday, November 14, 2013

Kilimo cha kahawa



Zaidi ya Baiskeli 100 zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 zimegawiwa kwa wakulima wa kahawa, wahamasishaji wa kilimo hifadhi pamoja na wakulima wawezeshaji  katika wilaya nne za Mkoa wa Mbeya zinazijihusisha na kilimo cha kahawa.

Meneja shughuli wa shirika la Hanns R. Neumann Stiftung Africa Ltd, Webster Miyanda alisema lengo la kugawa baiskeli hizo ni kuwawezesha wakulima na wahamasishaji wa kilimo hifadhi  kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku ambapo wakulima waliofadika ni wa wilaya za Mbeya, Ileje, Rungwe na Mbozi.