Wednesday, March 25, 2009

hii ni Tanzania bwana

Kwa taarifa yako hii ni Tanzania bwana, wakati wengine wakizima moto kwa kutumia kikombe cha maji, huku nyumba zao zikiwa hazina bima, kwa alijinyima kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kusimamisha nyumba hiyo iliyoungua kwa siku moja! Wengine wanaweza kubadilisha majina ya mitaa kama inavyoonekana hapa chini mtaa maarufu wa Kisutu Jijini Dar es Salaamumebadilishwa jina na kuwa 'Pramukh Swami' inachanganya lakini ndio Tanzania bwana

Tuesday, March 24, 2009

unamfahamu kiongozi anayetufaa

Mdau aliyejitambulisha kwa herufi 'R' anataja sifa za kiongozi. KIONGOZI ANAYETUFAA HUYU HAPA Kiongozi wa kweli:- ni mtumishi apendaye kwa hiari kuwatumika watu, siyo mtawala apendaye kwa ushawishi kutumikiwa na watu; Kiongozi wa kweli, maisha yake ni mfano tosha kwa kufuatwa na watu kwa hiari pasipo kujipendekeza au majigambo; Kiongozi wa kweli, hajinufasishi binafsi kupitia watu, bali ana uchungu wa shida za wengie na shauku ya kunufaisha maisha ya wengine Kiongozi wa kweli, ni matunda ya mtu yatokanayo na dhamira safi, tabia njema na upeo wa hali ya juu; Kiongozi wa kweli, ni msikivu, mwepesi wa kukiri mapungufu yake na hujiwajibisha mwenyewe pindi ashindwapo jambo pasipo visingizio; Kiongozi wa kweli, huwa tayari wakati wote kujifunza kutoka kwa watu wengine au jamii; Kiongozi wa kweli, hatofautishi kati ya maneno na matendo yake, siyo mnafiki wala kigeugeu Kiongozi wa kweli, hachukizwi na ushindani au upinzani bali huona ni changamoto na fursa pekee ya kujisahihisha na kujifunza ili kuelekea mahusiano bora na yenye faida kwa jamii. Kiongozi wa kweli, hapapariki wala kutapatapa apatwapo na matatizo, bali huwa jasiri na mwenye matumaini; Kiongozi wa kweli, hamiliki, hatawali wala hawi na amri juu ya watu, bali hushirikiana na kushauriana na watu anaowaongoza katika kuamua hatima yao na yake; Kiongozi wa kweli, hufurahia na kupongeza mafanikio ya wengine pasipo kuona gere na, husononeshwa na kusikitishwa na maanguko ya wengine Kiongozi wa kweli, mara nyingi haigi watu wengine, bali hubuni na kuvumbua mambo mapya yaliyo bora zaidi; Kiongozi wa kweli, wakati wote hutafuta maarifa, busara na hekima mpya na kamwe hathubutu kuhitimisha kujifunza katika maisha yake yote; Kiongozi wa kweli, hajilinganishi na wengine au kubweteka na mafanikio yake, bali hukazana kupanga na kutekeleza malengo na majukumu mapya anayojipangia kuelekea ubora endelevu na usiokoma kuboreka; Kiongozi wa kweli, wakati wote hurekebika, hukomaa, hukua na kujiendeleza kadri anavyoendelea kuongoza pasipo chembe yoyote ya ukaidi. Kiongozi wa kweli, huwa na mtazamo wa kuwajali binadamu wote waishio ulimwenguni, na hawi na mtazamo finyu usioona mbali.

Tukumbuke kidogo hili

kwa mataifa ya wenzetu kiongozi wa Kitaifa kushambuliwa si jambo dogo, lakini kwa hili la kupigwa kwa Mzee Ruksa linapaswa kuangaliwa vizuri kidogo, ni kweli tunafahamu kuwa ugonjwa wa ukimwi upo na mtu anaweza kuupata ikiwa atafanya ngono isiyo salama na kuwa na wapenzi wengi kwelikweli. Ili kuzuia maambukizi mapya wataalami wakabuni kondomu ambayo inasaidia kupunguza maambukizi mapya ya vvu kwa maana isipotumiwa kwa usahihi bado unaweza kuupata ukimwi hata kama umevaa kondomu. Hoja yangu, hivi misimamo ya dini na mtu mmoja mmoja inapaswa kuchukuliwa kama ndio msimamo wa Watanzania, ambaye hataki kutumia kondomu ni lazima aonyeshe msimamo wake kwa vurugu? Kijana Said akipokea kichapo baada ya kumchapa kibao mzee Ruksa.

Monday, March 16, 2009

Utaratibu wa kuficha ujumbe kwa bakora na vibao

Hii tabia hakika ni mbaya na wala haipendezi kabisa, dhana ya kuamini ujumbe hauwezi kufika kwa jamii bila kutumia viboko au kuchapa kiongozi kibaya ni ya hovyo na haifai kuigwa.
Tutafute namna bora ya kufanya hivyo, kueleza kero zetu na jinsi ya kuzipatia ufumbuzi na si mbinu mpya iliyobuniwa na aliyekuwa DC wa Bukoba, ndugu Mnali na sasa naona inaanza kupata waumini kwa kasi ya aina yake.

Saturday, March 14, 2009

wavuvi haramu

Baadhi ya Raia wa China na Indonesia ambao jana walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuendesha shughuli za uvuvi nchini bila ya kuwa na kibali kinyume na sheria za nchi na za Kimataifa. wote walikana mashitaka yao na kurudishwa mahabusu.

kwa Mujibu wa sheria, watuhumiwa hao wakikutwa na hatia watatakiwa kulipa faini ya shilingi bilioni 20, au meli waliyokuwa wanaitumia kufanya uvuvi haramu itataifishwa na kuwa mali ya Tanzania.

Namna ya Kukomesha wezi ktk ATM

Unaweza ukawa umeingia katika ATM machine kwa lengo la kujichukulia vijisenti vya matumizi wiki end hii, lakini ghafla jizi likakufuata na kukulazimisha uchukue fedha. Usibishane nalo maana laweza kukuzuru, unachotakiwa kufanya ni kuingiza namba zako za siri kinyume, kwa mfano namba yako ya siri ni 2009, unachofanya ni kuandika 9002, fedha zitatoka lakini nusu zitakwama kwenye machine na itapiga alam itakayowajulisha polisi bila jizi kujua hadi linakamatwa labda liwe janja likurupuke Mfumo huo umetengenezwa kwa lengo la kutoa msaada endapo kutatokea hatari yoyote.source Feedbitz

Friday, March 13, 2009

Watalii waionyesha kazi Simba

Kama ulidhani walikujakutalii nchini, umekosea timu ya Van couver kutoka Canada jana walionyesha kazi wekundu wa Msimbazi kwa kuwachapa magoli 2-1 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar, kumbuka Yanga waliwachapa Wacanada hao goli 3-0.

Matajiri wa Dunia

1. William Gates III (53) anaongoza kwa utajiri duniani akiwa na utajiri unaofikia thamani ya dola za Kimarekani bilioni 40, kibopa huyo ni baba wa watoto watatu, ambapo utajiri wake unatokana na microsoft
Kibopa anayemfuatia Bill Gates ni Warren Buffett (78) ambaye ana utajiri unaofikia dola za kimarekani bilioni 37, akiwa ni baba wa watoto watatu ambaye awali alikuwa na mke ambaye alifariki na akaoa mke mwingine, chanzo cha fedha kilichomuwezesha kuwa bilionea ni uwekezaji ndani ya Marekani. Wapo wengi hao ni wawili wa juu
Hao ni wenzetu wakati sie tunabishana juu ya ununuzi wa mitambo ya Dowarns, EPA na wale sijui eti walitumia vubaya ofisi zao na kulisababishia taifa hasara kubwa, wenzetu wanasonga tu, sie twakalia siasa

Thursday, March 12, 2009

Kwa kutuma msg huku hatari inakuja

Kweli Duniani kuna mambo, alianza Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Mnali kwa kuwacharaza bakora walimu wa shule ya Msingi Katerero kwa kile alichodai kuwa hawatimizi majukumu na hata akafikia hatua ya kusema kuwa anajua atafukuzwa kazi, lakini MESSAGE SENT na kweli akafukuzwa kazi. Kabla hatujakaa sawa, Kijana Ibrahim Said nae akamlamba kofi Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu na Kipenzi cha watu maarufu kama mzee ruksa naye anadai kuwa alikuwa anatafuta njia ya kufikisha ujumbe kupinga viongozi wa dini kuzungumzia kondomu na ushirikiano baina ya waislamu na wakristo. Soma hapa chini japo ufupi msikie aliyewahi kuwa RPC Mbeya na sasa Dar es Salaam anachozungumza. Kijana anayeshikiliwa kutokana na kumpiga kofi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitalini kupimwa akili huku Polisi ikiendelea kuchunguza kama anahusika na kikundi chochote cha wanaharakati wenye msimamo mkali. Wakati hatua hiyo ikichukuliwa, taasisi na watu mbalimbali wamelaani kitendo hicho cha kumpiga Rais mstaafu na kusema ni kinyume na maadili ya Watanzania. Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba kijana huyo, Ibrahim Said (26) aliiambia Polisi kuwa alifanya hivyo kutokana na kuchukizwa na hotuba zinazosisitiza Waislamu kushirikiana na Wakristo. Kova alisema kijana huyo alidai kwamba aliamua kumpiga kiongozi huyo mstaafu kwa sababu hakubaliani na hotuba za viongozi wa Kiislamu zinazosisitiza Waislamu na Wakristo kushirikiana katika kuadhimisha sikukuu za kidini kama vile Maulid, Idd (kwa Waislamu), Pasaka na Krismasi (Wakristo). Kwa mujibu wa Kova, Said alidai kuwa hakuwa na lengo lolote la kumdhuru Rais Mwinyi bali alikuwa akifikisha ujumbe kwa jamii. Kamanda Kova alisema alipohojiwa na Polisi, Said alisema anataka sikukuu za Kiislamu washerehekee kivyao na Wakristo washerehekee peke yao, wasilazimishwe kuwa na umoja. Pia Said alidai anapinga matumizi ya kondomu kwa kuwa watu wakitumia kondomu, watakuwa wamehalalisha uzinifu kwa Waislamu. Kova alisema kutokana na kitendo cha Said kumpiga Rais Mwinyi aliyekuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam juzi saa 12 jioni, alipelekwa jana Muhimbili kabla ya kufikishwa leo mahakamani.

Kutana na Mashabiki wa soka Duniani

Wednesday, March 11, 2009

Heshimaaaaa toa

Ni Vijana wakakamavu, lakini lipo jambo kidogo linasikitisha. Wakiwa kama watanzania wengine wenye ajira, askari wa kampuni binafsi za ulinzi ndio wanaolipwa kiduchu pengine kuliko hata house girl anayefanya kazi kwa kibosile.
Kwanza wanakesha wakilinda mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi, lakini hivi karibuni Chama cha makampuni ya ulinzi binafsi kilitangaza kuwa askari waliopo chini ya makampuni hayo watawajibika kuwalinda albino ili wasiendelee kuawa ingawa bado vitendo hivyo vya kinyama na kishenzi vinaendelea.
Sasa kuna swali huwa najiuliza, hawa walinzi wa sekta binafsi wengi wao mishahara yao ni kati shilingi 25,000 au 35,000 wanafamilia na watu wanaowategemea, kwa kuamua kuwalinda albino ni jambo jema sana,lakini nyie wamiliki hebu waongezeeni mishahara japo kidogo ili wasigeuka kuwa wezi katika maeneo wanayoyalinda.

Tuesday, March 10, 2009

Hongera

Rais Kikwete akimpongeza mwanamke pekee kutoka Afrika Kusini aliyeshiriki katika operesheni ya kuikamata meli ya wavuvi haramu.

Meli hii kuwa mali ya Tanzania?

Askari akilinda meli iliyokamatwa katika bahari ya hindi ikifanya shughuli za uvuvi haramu, hata hivyo meli hiyo haijulikani ni ya nchi gani huku mabaria karibu 30 waliokutwa ndani ya meli hiyo wakishindwa kuhojiwa kwa kile kilichodaiwa kuwa wanazungumza lugha ya ajabu na isiyo eleweka ni ya Taifa gani. ila jana kwenye TV niliwaona kama wakionyesha alama ya dole kwa wapiga picha wa tv.

Habari njema ni kuwa meli hiyo inaweza kuwa mali ya Tanzania ikiwa wamiliki wa meli hiyo watashindwa kulipa faini ya bilioni 20 ikiwa ni kosa la kuingia katika eneo la Tanzania kufanya shughuli za uvuvi haramu bila ya kuwa na vibali.

Yanga Bwana weee acha

Mshambuliaji Ben Mwalala wa Yanga akimtoka beki wa Vancover Whitecaps ya Canada, Trafford mason katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es salaam jana. Katika mchezo huo yanga iliibuka na ushindi mnono wa magoli 3-0, magoli hayo yaliwekwa kimiani na Jerry Tegete aliyepachika mawili na Mkenya Mike Baraza aliyemalizia la tatu.

Kweli Yesu anaweza

Muimbaji wa nyimbo za Injili, Ambele Chapanyota enzi hizo akiwa mmoja wa wakabaji na wezi katika eneo la nonde Jijini.
Baada ya kumpokea Bwana Yesu alibadilika na kuwa mtu mwema katika jamii na ndipo bwana Yesu akamfunulia na kumuonyesha kuwa ana kipaji cha uimbaji na sasa anatamba na Albamu inayokwenda kwa jina 'Salama kwa Yesu' kweli ukimfuata yeye ataukoa, atakubadilisha na kukupa maisha yenye amani duniani.
Akabarikiwa na kupata mke sasa ni mtu mwenye heshima yake, anawasihi vijana waache kutenda maovu kwa kuwa hayampendezi Mungu zaidi ya kuwafanya wawe na maisha ya hofu na kujificha kila wakati, kutengwa na jamii na kuogopwa kama mnyama. Kwake yeye hakuna linaloshindikana na wote tumfuate.

Monday, March 9, 2009

Ona tofauti hii

Tofauti ya tamaduni, ukitembelea visiwa vya Zanzibar ni kawaida kabisa kukutana na wanawake waliojitanda kanga na baibui mwili huku wengine wakiacha macho tu, lakini kwa kuwa visiwa hivyo vimejaliwa kuwa na fukwe nzuri, pia si ajabu kukutana na wanawake wa kizungu wakiwa wamevalia bikini na kanguo kadogo kwa juu kanaitwa sidiria. source Feedblitz

Biashara

Biashara ndogo ndio msingi wa maisha ya watanzania wengi hususani wanawake. ni biashara za machungwa, ndizi, mboga za majani na nyinginezo ambazo hata mtaji wake hauzidi shilingi 50,000,wengi wanaishi katika nyumba za kupanga huku wakiwa na familia zinazowategemea na wanasomesha watoto. Mikopo, Serikali na taasisi za fedha zimekuwa zikiwahamasisha wananchi kukopa ili waweze kuwa na miradi endelevu na inayoweza kuwainua kiuchumi, lakini riba za mikopo hiyo zimekuwa ni tishio na kusababisha wengi washindwe kukopa, pia wengi hawana vitu vya kuwekeza kama dhamana. Ipo haja kwa serikali kuweka mkakati utakaowasaidia watanzania wa kawaida kuwa na uwezo wa kupata mikopo.

Sunday, March 8, 2009

Nyama choma

aaaa kwa jumapili ya leo ukikaa sehemu yenye chama choma huku kukiwa na utulivu wa kutosha na unakamata kinywaji kile Unachopenda maisha yanakuwa matam, picha FeedBlitz

Ajali, Llori lagonga kipanya na kuua 4, 17 hoi

WATU wanne wamekufa wakiwemo watatu waliokufa papo hapo na wengine 17 kujeruhiwa vibaya baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace walilokuwa wakisafiria kutoka Tukuyu kuja Mbeya Mjini kugongwa kwa nyuma na lori la mizigo. Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 1:55 usiku katika barabara ya Tukuyu-Mbeya ambapo alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha magari matatu. Waliokufa katika ajali hiyo ambao wote walikuwa kwenye basi dogo la abiria kuwa ni pamoja na kondakta wa Toyota Hiace Martin Daimon, Daud Mwaigwiso, mtoto mdogo mwenye umri wa miaka miwili, James Msesa, na msichana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20-25 ambaye hajatambuliwa . Waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kuwa ni Eli Samson (7), Zainab Sege (45), Eda Kibinga (38), Angesisye Mbilinyi (32) wote wakazi wa kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe. Wengine waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Upendo Rashind (28), Deltha Mbogela (35),Telesia John (38), Hassan Ally (39), Elizabert Elia (31), Haruna Fungo (45), Elia Msenye (28), Ashel Mbilinyi (40), Hilda Kasewa (13) na Fatuma Kapusi, Tedy Msesa na Osca Kasewa Ajali yenyewe ilikuwa hivi, basi dogo la abiria lenye namba usajili T 568 AAE liligongwa kwa nyuma na lori la mizigo namba T 499 AJA likiwa na tela lake T 476 AJA aina ya Volvo, likiendeshwa na Ally Mohamed, lilikuwa limebeba karanga kutokea nchini Malawi kuelekea Uyole likiendeshwa . Kabla ya kuigonga kwa nyuma Toyota Hiace,Lori hilo lilianza kuligonga lori jingine la mafuta lenye namba za usajili T 283 ARE na tela lake no. T 668 ARA mali ya kampuni ya Dhandhoo lililokuwa likipeleka mafuta nchini Malawi. Hawa madereva wanafanya mzaha na roho zetu, tusiwaache watatumaliza Mwisho.

Harakati za maisha

Aaa baada ya kazi, lazima kupata kiburudisho japo kidoogo

Saturday, March 7, 2009

Wanaume kuhamishiwa Mimba

Mwene Mkuu wa Wasafwa wa wilaya ya Mbeya, Shao Soja Masoko akiwa na mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile wakati wa mkutano baina ya kiongozi huyo na wazee wa mila.
Mwakipesile akiagana na Chifu Mwashinga mara baada ya mkutano huo na chini ni baadhi ya machifu waliohudhuria mkutano huo, Sasa kama ulikuwa hujui kama mwanaume anaweza kupata mimba, soma hapa chini
Kwa wale wanaume wakwale, ambao hawapendi kuona sketi na vijisuruali vya mabinti hasa wanafunzi wakatize hivi, hadi wawatoe nguo katika guest na magetho kiama chao kinakuja.Wazee wa Mila wa kabila la wasafwa, wameiomba Serikali Mkoani Mbeya iwape kibali ili waweze kuwashughulikia wanaume wanaowapa mimba wanafunzi na kusababisha wakatize masomo huku wao wakidunda mitaani na kuwaacha mabinti hao na vitumbo bila msaada.
Mwene Mkuu, Masoko, alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kuwa wao wanakamati zao za ufundi na kama serikali ikiwapa kibali watawashughulikia wanaume wanaowajaza mimba wanafunzi kwa kuwahamishia katika matumbo yao na wanafunzi kuendelea na masomo kama kawaida, "yaani ipo hivi wewe, kwa mfano Juma umejifanya kidume unampa mimba Vanesa ambaye ni mwanafunzi, sasa hawa machifu kupitia darubini zao wanakuona wewe ndio muhusika, na kwa kutumia kamati ya ufundi wanachukua hiyo mimba na kuiweka katika tumbo lako'
Lakini wazee wa mila hao wakasonga mbele zaidi na kusema wapiga nondo nao wakae tayari tayari kwa kuwa kupitia darubini zao watawaona na kuwatengua miguu, kuwafanya wajipeleke polisi na walio na viungo vya binadamu watajitokeza hadharani wakiwa wamevibeba na polisi kuwakamata kiulaini kama wananawa. Habri ndio hiyo tukae mkao wa kula tukisubiri kuona wanaume wakiwa na mimba na si vitambi tena.

Friday, March 6, 2009

Wanafunzi nusura wamacharaze bakora Mkuu wao wa shule

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nzondahaki iliyopo katika Kata ya Nzovwe Jijini Mbeya, Ritha Mtweve juzi alinusurika kupigwa viboko na wanafunzi wa shule hiyo, kwa madai kuwa amekuwa akiwatolea lugha chafu pamoja na kutowasomea taarifa ya miradi ya elimu ya kujitegema. Katika vurugu hizo, wanafunzi hao wa kidato cha kwanza hadi cha tatu waliokuwa wamebeba mawe na fimbo walivunja madirisha kwa mawe, kuwajeruhi walimu wawili pamoja na kuwacharaza bakora wanafunzi wenzao waliogoma kushiriki katika vurugu hizo. Wanafunzi hao waliokuwa wamejaa mchecheto, huku wakishangilia na kupiga makelele wakiwa wamebeba mawe na bakora waliwaamuru walimu wengine warudi majumbani kwao na wamuache mkuu wa shule hiyo hali ambayo iliwatia hofu walimu na kuamua wote kubaki na kujifungia ofisini Kitendo cha walimu wengine kugoma kuondoka kiliwapandisha jazba na kuanza kurusha mawe ambapo waliwajeruhi walimu wawili. Hii ni inakumbusha katika shule ya Katerero Mkoani Kagera ambapo walimu walikuwa bakora kwa amri ya dc, lakini hawa wanafunzi walitaka wamchampe mkuu wa wao kwa lugha chafu, kutosoma taarifa na ukosefu wa vitabu

Burudani

Ni burudani ya muziki, tu binti tukionyesha ufundi wa kukata viuno mbele ya mamia ya wakazi wa Jiji la Mbeya waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa label mpya ya bia ya Castle
Utamu wa burudani ulipozidi, almanusra wasahau kudhibiti nguo zao, ambazo zilikuwa na dalili ya kuanza kuwashuka mwilini, burudani bwana inautamu wake

Thursday, March 5, 2009

Wafahamu watangazaji wa Mbeya fm redio

Mtangazaji wa Mbeya fm Redio akiwa kazini
Timu ya watangazaji ya Mbeya fm redio wakiwa katika picha ya pamoja kwa pozi tofauti na tabasamu pana

Wednesday, March 4, 2009

Breaking news:mvua yaleta madhara Rungwe

Mvua kubwa iliyonyesha katika katika eneo la Kibumbe Kiwira wilayani Rungwe imeangusha nyumba tisa, nguzo za umeme, miti na migomba, lakini hadi sasa hakuna taarifa ya kuwepo majeruhi wala vifo kwa wanaoishi katika nyumba hizo.

Ujambazi wa kutumia silaha waibuka tena Mbeya

Wale majambazi waliokuwa wanatamba na kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha wameibuka tena. Kundi la Watu 10 wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa wamebeba silaha na nondo juzi usiku walivamia kiwanda cha nguo (Mbeya Textile) kilichopo Songwe wilaya ya Mbeya na kuiba sefu ya kuhifadhia fedha, kuwajeruhi walinzi watatu, kuwapora bunduki tatu ikiwamo shortgun moja na kukimbilia kusikojulikana. Majambazi hao wanaoonekana wababe wakiwa na silaha na nondo, walivamia kiwanda hicho majira ya saa 8 usiku na kuwaweka chini ya ulinzi, walinzi watatu waliokuwa wamebeba bunduki tatu, mbili rifle na shortgun moja. Kwa habari kamili kesho

Tuleteeni Matrekta Jamani

Kiukweli Matrekta yanahitajika sana hasa katika maeneo ya vijijini ili wananchi waondokana na kilimo cha kutumia zana zaifu na ambazo hazileti tija, japo kwa kutumia wanyama kazi kunasaidia kuboresha kilimo lakini bado mkulima inabidi asaidiwe ili aweze kufikisha mazao yeye mwenyewe sokoni badala ya kumtumia mtu wa kati (Middle man) ambaye ndiye mfaidika mkuu kuliko mvuja jasho.
Ili watoto kama hawa wapate elimu bora na maisha safi wakulima wanahitaji kusaidia

Tuesday, March 3, 2009

Rais, Mkuu wa Majeshi Guinea wauawa

Askari waasi wamemuua kwa risasi Rais Joao Bernardo Vieira, maofisa wa serikali wamesema. Habari hizo zilikuja jana saa chache baada ya mauaji ya mkuu wa majeshi ambaye alikuwa katika mtafaruku na Rais. Milio ya risasi ilisikika jijini hapa na mpaka leo hakukuwa na taarifa za nani anaiongoza serikali. Nchi hii ni moja ya nchi masikini sana duniani, na ina historia ya mapinduzi ya serikali na imekuwa njia kuu ya dawa za kulevya, hususan kokeni kwenda Ulaya. Taarifa ziliwakariri maofisa wa kijeshi na serikali waliosema Rais ameuawa. "Rais Vieira aliuawa na Jeshi alipokuwa akijaribu kukimbia makazi yake ambayo yalishambuliwa na kikundi cha wanajeshi watiifu kwa aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Tagme Na Waie, mapema asubuhi hii," msemaji wa Jeshi, Zamora Induta aliiambia AFP. Alimtuhumu Rais Vieira kwa kuhusika na mauaji ya mkuu wa majeshi. Jenerali Tagme aliuawa baada ya mlipuko kusikika juzi na kuharibu sehemu ya makao makuu ya jeshi. Msaidizi wake, Luteni Kanali Bwam Nhamtchio, alisema Tagme alikuwa ofisini mlipuko huo ulipotokea. "Alijeruhiwa sana asingeweza kupona. Hili ni pigo kwetu sote," alisema Nhamtchio. Takriban watu watano waliripotiwa kuuawa na mlipuko huo. Kutokana na mashambulizi hayo dhidi ya makao makuu ya Jeshi, maofisa waliviamuru vituo viwili vya redio kusitisha matangazo. "Kwa usalama wenu waandishi wa habari, fungeni kituo na kuacha kutangaza. Ni kwa usalama wenu," msemaji wa Jeshi Samuel Fernandes aliwaambia waandishi wa habari katika moja ya vituo hivyo. "Tunakwenda kupambana na wavamizi na kujilinda," aliongeza.

Huku nako ni Tanzania

Huku nako wapo Watanzania wanaishi, ni maeneo ya wilayani Mbozi vijijini

Monday, March 2, 2009

Hata vijijini

Kama ulidhani Arsenal 'Washika Bunduki' wana mashabiki mijini tena watu wazima tu, sahau hilo, hata watoto wa vijijini na mijini naowamo

Sunday, March 1, 2009

wape nafasi ya masomo

Wape nafasi watoto wa Kike wasome, kazi kama hizi zinawafanya washindwe kukua vizuri kiakili na kimwili na hivyo kudunisha uwezo wao wa kutenda na kufikiri