

Ugumu wa maisha umesababisha vijana watumie mbinu mbalimbali katika kusaka fedha zitkazowawezesha kumudu maisha ya kila siku. Picha ya Juu, baadhi ya wapiga picha wakiwa katika harakati za kupiga picha za katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine, wawahi studio kusafisha na kurudi kuziuza kwa mashabiki wa soka.
Picha ya pili, waliokuwa Mawakala wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakiwa nje ya ofisi za Chama hicho zilizopo Mbalizi wakishinikiza walipwe posho ya shilingi 10,000 waliyoahidiwa.
Vijana ni moja ya rasimali muhimu kwa Taifa lolote, na ili Taifa liweze kupata maendeleo linahitaji vijana kwa kuwa ndio nguvu kazi ya Taifa. Je Vijana wa Kitanzania wakiwemo wasomi wa vyuo vikuu, wasomi wa kawaida na wale waliopo Mitaani wanatumika ipasavyo, nini kifanyike ili vijana waweze kuwa na maisha bora.
No comments:
Post a Comment