Kupitia blog hii utapata nafasi ya kuyajua mambo yanayojiri kila siku katika Mkoa wa Mbeya zikiwemo, habari mbalimbali zinazohusu jamii, matukio, na tetesi mbalimbali. Pia kupitia blog hii tutajadili masuala mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Mkoa wa Mbeya.
Tuesday, November 16, 2010
Breaking News
Mizengo Peter Pinda ndiye waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2010-2015, mtoto wa mkulima kutoka katika jimbo la Katavi Mkoa mpya wa Katavi.
Monday, November 8, 2010
Breaking news
Haile Gebrselassie(37) rasmi amejiuzulu katika mbio za marathon baada ya mguu wake kupata hitilafu katika mbio za marathon New York, anasema anafikiria kuingia katika siasa lakini kabla ataangalia namna ya kuwasaidia wananchi wa Ethiopia. mfukuza upepo huyo anamiliki shule mbili, ni wakala wa kuuza magari, hoteli na biashara kadhaa ambazo zimetoa ajira kwa Raia wa Ethiopia
Wednesday, October 27, 2010
Pweza Paul afariki
Pweza Paul aliyeondokea kuwa mtabiri maarufu katika michuano ya Kombe la dunia 2010, amefariki.
Paul amefariki kifo cha kawaida, ambapo kwa mujibu wa wataalam, Pweza huishi kwa wastani wa miaka miwili na nusu na Pweza Paul alikuwa tayari katika umri umri
Tuesday, October 19, 2010
Monday, October 18, 2010
Siasa
Thursday, October 14, 2010
Mama na mtoto
Wednesday, October 13, 2010
Vijana
Tuesday, October 12, 2010
Uwindaji
Monday, October 11, 2010
Kwa taarifa yako
Mitaani kwetu
Monday, September 27, 2010
ajali ya mwenyekiti
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya,(MBPC), Nico Mwaibale pamoja na mkewe pamoja na Katibu Mkuu wa MBPC, Patrick Kossim na abiria mwingine ambaye hajafahamika jana walinusurika kufa baada ya gari yao kupata pancha tairi la nyuma, katika eneo mafinga na gari yao kutumbukia kolongoni , lakini wote ni wazima, gari imetolewa korongoni linarudishwa Mbeya kwa matengenezo na majira ya saa 10 hivi walikuwa wanajiandaa na safari ya kuelekea DSM, sasa kwa basi na si kwa gari binafsi tena
Saturday, May 22, 2010
Hawa nao ni watoto wa Kitanzania
Hawa nao ni watoto wa Kitanzania waliopo Iganjo uyole Jijini Mbeya, watoto hawa nao wapo Tanzania na ni watanzania, hapa walikuwa wametoka kuogelea katika mto na kukutana na baadhi ya waandishi waliokuwa wametembelea mradi wa umwagiliaji wa Iganjo.
Mwandishi wa Baraka FM ya Jiji Mbeya akizungumza na mmoja wa watoto huku mwenzake akifanyajitihada za kuhakikisha suruali yake isimdondoke.Uwezeshaji kiuchumi wananchi utasaidia kuboresha maisha sawa kwa watoto wote na wao kuweza kumudu kusoma katika shule bora,kuishi maisha bora kama ilivyo kwa watoto wengine.
Friday, May 21, 2010
Tutapona kweli
Wakulima wa Bonde la Uyole wakisafisha karoti katika mto ulio karibu na daraja la Igawilo nje kidogo ya Jiji la Mbeya.Baadhi ya watu wanatabia ya kula karoti zikiwa hazijaoshwa mara baada tu ya kununua kutoka sokoni. Ofisi ya Mkemia Mkuu imefunguliwa Mbeya ni nafasi ya ofisi hiyo kuchunguza kama maji hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu.
Thursday, May 20, 2010
Kilimo Kwanza na waandishi
Wednesday, May 19, 2010
Ofisi ya Mkemia Mkuu sasa Nyanda za Juu Kusini
Kwa wale wenye tabia ya kupachika mimba wanafunzi, wanaokataa au kusingiziwa watoto, kubaini wanaohusika na mauaji ya watoto na uchunaji ngozi pamoja na uchunguzi wa kisayansi kama kwa maji ya kisima na mengine. Sawa dawa ipo sebuleni na si jikoni tena Baada ya Mkemia Mkuu kufungua ofisi kwa Mikoa ya Nyanda za Juu kusini.
Wananchi tutumie fursa hii kwa ajili ya utatuzi wa mambo mbalimbali yanahusiana na tafiti za kisayansi.Tuelewe kuwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali si kwa ajili ya kushughulikia masuala ya jinai tu
Monday, May 17, 2010
Siku ya familia Duniani
Jumamosi, May 15, nilibahatika kuhudhuria maadhimisho ya siku ya familia Duniani ambayo Jijini Mbeya yaliazimishwa katika viwanja vya shule ya msingi Nzovwe, kwa umuhimu wa siku yenyewe iliyoandaliwa na taasisi ya Champion nilitaraji wazazi wangehudhuria kwa wingi, lakini idadi ya watoto ilikuwa kubwa huku matumizi ya kondomu yakihimizwa
Sunday, March 21, 2010
Mmmh Miss wetu
Saturday, March 20, 2010
usafiri wetu
Saturday, March 6, 2010
Mama na Mtoto
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya filauni, ni huko Cambridge, Uingereza Mtoto Xavier King (pichani) aliwaacha watu vinywa wazi baada ya kuanza kutembea bila kutambaa tofauti na hatua za ukuaji wa kawaida wa mtoto.
Mtoto huyo ambaye Februari 15, mwaka huu alitimiza miezi sita, alinyanyuka ghafla wiki moja kabla ya siku hiyo na kutembea akiwa ameshika ukuta. Hiyo ilikuwa hatua yake ya kwanza ya kuanza kutembea bila msaada wowote. Hatua hiyo haikuwashangaza sana wazazi wake, kwani waliamini kwamba alikuwa akicheza, ikizingatiwa kuwa mara kwa mara alikuwa akianguka. Siku mbili baadaye, mtoto huyo alianza kutembea bila kushika popote., mara hiyo akifanya hivyo kwa umbali wa futi sita kutoka mahali anapokuwa. Hapo ndipo alipowashangaza wazazi wake. “Sikuwa na mawazo hayo na kamwe sikuwahi kufikiria jambo la ajabu la aina hiyo. Kama mzazi niliishia kushangaa, nilimpigia simu baba yake kazini na kumwabia, naye alishangaa, “ anasema mama wa mtoto huyo, Mary King (30).
Mzazi huyo ambaye ni muuguzi anasema, watoto wengi huweza kutembea baada ya kufikisha miezi 10 ama mwaka mmoja.
Sunday, February 28, 2010
Subscribe to:
Posts (Atom)









