Wednesday, February 18, 2009

Mwanafunzi afa akimkimbia

Mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Sekondari ya mchanganyiko ya Mwakaleli wilayani Rungwe, amefariki dunia jana baada ya kujigonga, kupasuka sehemu ya paji la uso wakati walipokuwa wakiwakimbia Walimu. Mwanafunzi huyo Edson Mwanjali (20), alifariki jana alipokuwa akipatiwa matibabu jana katika hospitakli ya Rufaa Mbeya. Chanzo chake.Februari 14 majira ya saa 2 usiku, Mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo, John Lazaro (27) akiwa na mwalimu mwenzake Mwete Wilson, waliwa katika ukaguzi wa kawaida wa kukagua nidhamu ya wanafunzi wa shule hiyo ambao ni mchanganyiko wa wavulana na wasichana. Wakiwa wanakatiza katika mitaa ya shule hiyo, ghafla wakaona wanafunzi wakiwa kwenye uwanja wa shule hiyo, na kuamua kwenda kushuhudia ili kuyafanya macho yao yaamini kama ni kweli wameona, lakini wakiwa wanajimuvuzisha, wanafunzi walishitukia mwanga wa kurunzi na kuamua kutimua mbio na hatima Mwanjali kuishia kujigonga katika mwamba wa goli la chuma na hatimaye kufariki kufariki Februari 17. Maswali ya kujiuliza, hawa wanafunzi wamekwenda Sekondari ya mwakaleli kwa ajili ya kusoma, lakini je? uwanjani walikuwa wanafanya nini usiku tena wavulana kwa wasichana. Nao Walimu walikuwa wanatembea tu ama walianza kutimua vumbi ili kukamata japo mwanafunzi mmoja kwa ushahidi. Polisi wanawashikilia walimu hao kupisha uchunguzi na kwa usalama wao maana wanafunzi walirusha mawe kabla ya kuzuiwa na risasi za polisi.

No comments:

Post a Comment