Thursday, February 5, 2009

Prison-ni kweli wanamuhitaji Mwambusi

Pichani: moja ya mashambulizi yaliyoelekezwa langoni kwa Prison katika mchezo uliochezwa katikauwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine na Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Timu ya Tanzania Prison, katika msimu uliopita ilianza ligi kwa kishindo na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa ya pili na kufanikiwa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, wakati huo ulikuwa ikinolewa na kocha Juma Mwambusi.
Ikiwa juu ya mafanikio timu hiyo iliamua kuachana na Mwambusi kwa kile kilichodaiwa kutofikia makubaliano ya kimaslahi na kuamua kumkabidhi mikoba mchezaji wa siku nyingi wa timu hiyo James Nestroy na kumrejesha timu Meneja Hassan Mlwilo.
Kilichotokea, tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom timu hiyo imeshindwa kutamba, katika mzunguko wa pili imepoteza mechi nne mfululizo,tatu za ligi kuu na moja ya Kimataifa. timu hiyo pekee inayowakilisha Mkoa wa Mbeya imepoteza muelekeo na dalili zake si njema.
Tukiwa wadau wa soka je ni kweli pengo la Mwambusi linaonekana katika timu hiyo? au ndio mwanzo wa timu hiyo kuelekea kupotea katika medani ya soka? nani mchawi wa prison, viongozi, makocha au wachezaji wenyewe?

No comments:

Post a Comment