Monday, October 5, 2009

Kombe la Duniani la Vijana wazururaji laja 2010

Kombe La Dunia La Vijana Wazururaji 2010:Tanzania Imo Tanzania ni miongoni mwa mataifa ambayo yatashirikishwa katika mashindano ya soka ya Kombe la Dunia, kwa vijana wanaozurura ovyo mitaani, yatakayofanyika mjini Durban, Afrika Kusini, mwezi Machi mwaka 2010. Mbali na wenyeji, mataifa mengine yatakayoshiriki ni Brazil, India, Nicaragua, Ufilipino, Ukraine, Uingereza na Vietman. Jumanne ya tarehe 22 Julai 2009, meneja wa chuo cha michezo cha watoto kutoka Mwanza,Tanzania, Bw Mutani Yangwe, alishiriki katika kikao mjini London kuzungumzia juu ya mashindano hayo ya dunia, na vile vile juu ya mipango ya Arsenal, klabu ya Uingereza, kukisaidia chuo hicho. SOURCE: BBC SWAHILI SERVICE.

Saturday, October 3, 2009

Kwa taarifa yako

Kwa tulio wengi lugha ya Kiingereza ni Tatizo, na tukifike kwenye mitumba tunababe nguo tu bila kuzingatia maana ya maneno yaliyomo kwenye fulana tunazovaa hebu soma maandishi katika fulana ya kijana na utakari ungekuwa wewe
unaweza usiamini lakini hii ndio Tanzania bwana na ndoto ya maisha bora kwa kila Mtanzania (source jamii forum)

Friday, September 25, 2009

Ludewa

natumai wote muwazima na mnaendelea vyema na shughuli za kila siku. Niwaombe radhi kwa kushindwa kuweka vitu vipya kila siku. Kuna mdau alivutiwa na picha za watoto wa Ludewa ambao walikuwa kipokea misaada ya nguo na baiskeli na akavutiwa na kuiona kuwa kuna haja ya yeye kwenda kutoa msaada kwa watoto hao. Ninachoweza kumshauri ni kuwasiliana moja kwa moja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa, na kwa ushauri ikiwa mdau anahitaji kufika hadi manda aende kipindi cha kiangazi kwa kuwa mvua zikianza kwa mujibu wa wenyeji hakufikiki kwa urahisi. Asante

Tuesday, August 11, 2009

Mambo ya Send ya Off

Ni mambo ya send offfice, kushoto ni Bibi Harusi aliyekuwa anaagwa kwa ajili ya kufunga ndoa na Mwandishi wa Habari wa Star Tv na RFA, Fred Bakalemwa, kulia ni Mpambe wa Bi Harusi, Brandy Nelson ambaye ni mwandishi wa gazeti la Mwananchi.
Mchungaji akiongoza misa wakati wa mchakato wa kumuaga bi harusi
Hii ni kudhihirisha furaha ya wazazi wa bi harusi ambao walijikuta wakiselebuka na kukumbuka enzi zao.
Bwana Harusi akitasabasamu huku akiwa na mpambe wake, Danny Tweve
Ndoa bwana, hapa bwana na bi harusi wakifanyiana mzaha wakati wa kupata mlo

Saturday, August 8, 2009

Kwa nini wanaume tu wapenda

Kwa nini wanaume tu! WAPENDE Kwa nini wanaume tu! .............. Wapendeni wake zenu kama Kristo anavyolipenda kanisa!Biblia ipo wazi kabisa na imetoa tamko zaidi ya mara 4 kwa mume kumpenda mke wake. Wakati huohuo mwanamke ameariwa mara moja tu kumpenda mume wake ingawa shughuli kwake ni kumtii mume. Kwa nini Biblia imesisitiza zaidi ya mara nne mwanaume kumpenda mke na mara moja tu mke kumpenda mume na kumtii? Hili ni swali ambalo limekuwa linaniuumiza kichwa na katika kuchunguza naamini sababu zifuatazo ni muhimu sana. Kwanza mwanamke anauhitaji mkubwa wa kupendwa, kuwa na mwanaume ambaye anampenda, anamjali, anamsikiliza na kujiona yupo katika mikono salama, nilikutana na mwanamke mmoja ambaye alilalamika kwamba “Without love I have no life” wanawake wengi hujikuta katika njia panda wakiwa ndani ya ndoa na mume aliyenaye haoneshi upendo wowote na kujali. Pili, wanaume tumekuwa na wakati mgumu sana kupenda kwa kumaanisha. Ukisikiliza mifano mbalimbali ambayo wanaume wamekuwa wanawadanganya wanawake unaweza kufika mahali ukajiuliza hivi akili za mwanamke huwa zinakuwa zimehama au ndo raha ya kupendwa! Kiasili mwanamke amekuwa na capacity kubwa kuhusiana na mapenzi (upendo au kupendwa) kuliko mwanaume. Mwanamke akisema amekupenda anakuwa amekupenda kwanza kwa kukuweka ndani ya moyo wake, wakati mwanaume kupenda kwake ni kwa vipande inawezekana amekupenda kwa sababu ya mguu tu basi na anaweza kukuahidi kukununulia gari na wewe ukakubali. Na kuna wakati wanawake wamekuwa wakijiuliza hivi wanaume tuna feelings au hatuna, kwani kuna wakati tunaweza kuwa kama “animals” kwa matendo yetu na vitu tunafanya kwa hivi viumbe “wanawake”, tunajilinda kwa kusema kwamba nao wepesi mno kudanganywa! Hata hivyo ni ngumu sana au ni mara chache sana kusikia mwanaume amejidhuru au kujiua baada ya kuachwa na mpenzi wake wa kike ingawa ni mara nyingi tunasikia mwanamke (hasa binti wa miaka 15 – 25) amejiumiza au kujiua kama si kuchanyanyikiwa kwa kumpoteza mpenzi wake wa kiume. Ni mara chache sana kukutana au kumuona mwanamke ambaye ameamua kuachana na mwanaume anayejua kupenda na kumpa mahitaji yake yote ya emotions kwani mwanamke akipata hitaji la kupendwa au husia za kupendwa hapo ndo ugonjwa wake umepata tiba, pia ni mara chache sana kukutana na mwanamke anayeomba msaada wa ushauri kwa ajili ya mwanaume ambaye anamjali sana kwenye ndoa yake. References: Ephesians 5:25 Ephesians 5:28-33 I Peter 3:7 Colossians 3:19 Proverbs 31:28-29

Friday, August 7, 2009

Ludewa bwana

Wakati huku mijini watoto wanashinda kwenye luninga, huku wengine wakitanua katika magari ya familia zao, huko Manda wilayani Ludewa kando kando kabisa ya ziwa nyasa, miundo mbinu mibovu na kusikofikika wakati wa mvua, watoto walikuwa hawajawahi kuona Baiskeli na shirika lisilo la Kiserikali la Cocoda la MkoaniIringa linaloshughulika na watoto yatima na wanaoishi katika mazingirsa magumu lilipeleka Baiskeli na vitu vingine, watoto walizizunguka huku wakizishangaa
Ni kama hawaamini kile wanachokiona, wao wanajua mitumbwi tu hakuna zaidi

aaaaa Ludewa

Hivi karibuni nilibahatika kutembelea wilaya ya Ludewa Mkoani Iringa hii ikiwa ni mara yangu ya kwanza kabisa na hasa kufika Manda kandokando ya ziwa nyasa, yapo mengi niliyojifunza na mengine si ya kujivunia hata kidogo. Cha kwanza ukiwasili Ludewa mjini na jioni wakati ukiwa unapata chakula au kinywaji kidogo si ajabu kufuatwa na msichana akaomba umnunulie soda na kuuliza umefikia wapi (akimaanisha guest), akiona unachelewa kumjibu pengine kwa kupigwa butwaa, ataongeza na jingine, "nasikia baridi unataka kunikumbatia?" bila hofu. Kwa sisi wageni tulishangaa lakini wenyeji wakatuambia aaa hiyo ni kawaida kabisa, sijui ukiwa wewe utafanyaje na ukizingatia na huu ugonjwa wa ukimwi. Mengi utayapata katika picha.

Friday, July 31, 2009

Vituko vya wakubwa

Kweli hakuna ambaye hapendi pale mahala, Hata mzee Ruksa aliwahi kusema kuwa '...............tena limekaa pale ambapo sote twapapenda.........' akimaanisha ugonjwa wa ukimwi. Hebu mtizame Mr. Obama hapa kumbe naye...............sema mwenyewe.
Muangalie na hapa tena, lahaula mzee kachanganyikiwa

Wasalaam

Ndugu wadau, kwa kipindi ch takribani miezi minne sikuweza kuweka vitu vipya kutokana na kukabilina na majukumu ya Kitaifa, lakini kuanzia sasa narudi tena naomba ushirikiano katika kutoa michango mbalimbali itakayotujenga

Friday, April 17, 2009

Big Psalm abatizwa, ilikuwa Pasaka

Hapa ilikuwa ni siku ya Pasaka, ambapo Big Psalm alibatizwa rasmi na Padri Mapunda wa Kanisa la Anglikana usharika wa Isanga, ambapo baada ya ubatizo Psalm akiwa na kundi lukuki la wajukuu wa Mzee Mng'ong'o walikwenda nyumbani kwa ajili ya shughuli za sherehe, anbapo siku hiyo watoto wengine wawili akiwemo wa baba yake Mkubwa Big Psalm alibatizwa.
Big Psalm akifurahia burudani ya show ya muziki ilikuwa ikiporomoshwa na watoto na wageni waalikwa "show yenyewe utishuhudia hapo chini"
Big Psalm akipiga makofi baada ya kufurahishwa na burudani iliyokuwa ikiporomoshwa na wacheza shoo "utawaona chini", hapa kilichomfurahisha ni wimbo wa jipange sawa sawa.
Big Psalm akifurahia jambo,
Big Psalm akijishika kichwa baada ya kukumbuka kuwa amesahau jambo la muhimu sana, wote tulipigwa na butwaa na kujiuliza ana nini.
Kumbe alisahau kupiga simu ya muhimu, hapa alikuwa tayari amenyang'anya simu ya Baba yake na kuwasiliana na mtu alikuwa anataka kumpigia, hakuna aliyejua ni nani huyo, mama watu wote muhimu walikuwepo.
Hapa akijadiliana jambo na mama yake mara baada ya kupiga simu hiyo.
Hapa Psalm kidogo ni kama alikuwa amezubaa huku mama yake akimtizama usoni, sijui walikuwa wamejibizana nini.
Hii ndiyo ile burudani uliyokuwa ukiisubiri kwa hamu, hapa wajomba na shangazi zake Psalm wakionyesha umahiri katika kusakata muziki wa injili,
Baba yake Mkubwa Psalm aliye kulia na Bibi yake mdogo hawakuwa nyuma katika kuonyesha ufundi wa kucheza nyimbo za injili kama wanavyoonekana picha ya juu na ya chini.
Hapa chini ni baadhi ya wageni waalikwa waliokuwa wakienda kutoa zawadi baada ya kupata burudani murua nyumbani kwa nyanya yake Psalm
Big Psalm bwana hata bado hajaondoka meza kuu tayari anataka kuanza kufungua zawadi na kubaini kilichomo ndani
Psalm vipi bwana, hapa alikuwa akiendelea na hekahela na kuhakikisha anafungua box la zawadi
Hapa uncle zake Pslam wakiwaaga nyanya zake Psalm ikiwa ni ishara ya kumaliza shughuli hiyo iliyokuwa ndogo lakini ilifana na kupendeza sana

Wednesday, March 25, 2009

hii ni Tanzania bwana

Kwa taarifa yako hii ni Tanzania bwana, wakati wengine wakizima moto kwa kutumia kikombe cha maji, huku nyumba zao zikiwa hazina bima, kwa alijinyima kwa miaka kadhaa na kufanikiwa kusimamisha nyumba hiyo iliyoungua kwa siku moja! Wengine wanaweza kubadilisha majina ya mitaa kama inavyoonekana hapa chini mtaa maarufu wa Kisutu Jijini Dar es Salaamumebadilishwa jina na kuwa 'Pramukh Swami' inachanganya lakini ndio Tanzania bwana

Tuesday, March 24, 2009

unamfahamu kiongozi anayetufaa

Mdau aliyejitambulisha kwa herufi 'R' anataja sifa za kiongozi. KIONGOZI ANAYETUFAA HUYU HAPA Kiongozi wa kweli:- ni mtumishi apendaye kwa hiari kuwatumika watu, siyo mtawala apendaye kwa ushawishi kutumikiwa na watu; Kiongozi wa kweli, maisha yake ni mfano tosha kwa kufuatwa na watu kwa hiari pasipo kujipendekeza au majigambo; Kiongozi wa kweli, hajinufasishi binafsi kupitia watu, bali ana uchungu wa shida za wengie na shauku ya kunufaisha maisha ya wengine Kiongozi wa kweli, ni matunda ya mtu yatokanayo na dhamira safi, tabia njema na upeo wa hali ya juu; Kiongozi wa kweli, ni msikivu, mwepesi wa kukiri mapungufu yake na hujiwajibisha mwenyewe pindi ashindwapo jambo pasipo visingizio; Kiongozi wa kweli, huwa tayari wakati wote kujifunza kutoka kwa watu wengine au jamii; Kiongozi wa kweli, hatofautishi kati ya maneno na matendo yake, siyo mnafiki wala kigeugeu Kiongozi wa kweli, hachukizwi na ushindani au upinzani bali huona ni changamoto na fursa pekee ya kujisahihisha na kujifunza ili kuelekea mahusiano bora na yenye faida kwa jamii. Kiongozi wa kweli, hapapariki wala kutapatapa apatwapo na matatizo, bali huwa jasiri na mwenye matumaini; Kiongozi wa kweli, hamiliki, hatawali wala hawi na amri juu ya watu, bali hushirikiana na kushauriana na watu anaowaongoza katika kuamua hatima yao na yake; Kiongozi wa kweli, hufurahia na kupongeza mafanikio ya wengine pasipo kuona gere na, husononeshwa na kusikitishwa na maanguko ya wengine Kiongozi wa kweli, mara nyingi haigi watu wengine, bali hubuni na kuvumbua mambo mapya yaliyo bora zaidi; Kiongozi wa kweli, wakati wote hutafuta maarifa, busara na hekima mpya na kamwe hathubutu kuhitimisha kujifunza katika maisha yake yote; Kiongozi wa kweli, hajilinganishi na wengine au kubweteka na mafanikio yake, bali hukazana kupanga na kutekeleza malengo na majukumu mapya anayojipangia kuelekea ubora endelevu na usiokoma kuboreka; Kiongozi wa kweli, wakati wote hurekebika, hukomaa, hukua na kujiendeleza kadri anavyoendelea kuongoza pasipo chembe yoyote ya ukaidi. Kiongozi wa kweli, huwa na mtazamo wa kuwajali binadamu wote waishio ulimwenguni, na hawi na mtazamo finyu usioona mbali.

Tukumbuke kidogo hili

kwa mataifa ya wenzetu kiongozi wa Kitaifa kushambuliwa si jambo dogo, lakini kwa hili la kupigwa kwa Mzee Ruksa linapaswa kuangaliwa vizuri kidogo, ni kweli tunafahamu kuwa ugonjwa wa ukimwi upo na mtu anaweza kuupata ikiwa atafanya ngono isiyo salama na kuwa na wapenzi wengi kwelikweli. Ili kuzuia maambukizi mapya wataalami wakabuni kondomu ambayo inasaidia kupunguza maambukizi mapya ya vvu kwa maana isipotumiwa kwa usahihi bado unaweza kuupata ukimwi hata kama umevaa kondomu. Hoja yangu, hivi misimamo ya dini na mtu mmoja mmoja inapaswa kuchukuliwa kama ndio msimamo wa Watanzania, ambaye hataki kutumia kondomu ni lazima aonyeshe msimamo wake kwa vurugu? Kijana Said akipokea kichapo baada ya kumchapa kibao mzee Ruksa.

Monday, March 16, 2009

Utaratibu wa kuficha ujumbe kwa bakora na vibao

Hii tabia hakika ni mbaya na wala haipendezi kabisa, dhana ya kuamini ujumbe hauwezi kufika kwa jamii bila kutumia viboko au kuchapa kiongozi kibaya ni ya hovyo na haifai kuigwa.
Tutafute namna bora ya kufanya hivyo, kueleza kero zetu na jinsi ya kuzipatia ufumbuzi na si mbinu mpya iliyobuniwa na aliyekuwa DC wa Bukoba, ndugu Mnali na sasa naona inaanza kupata waumini kwa kasi ya aina yake.

Saturday, March 14, 2009

wavuvi haramu

Baadhi ya Raia wa China na Indonesia ambao jana walipandishwa kizimbani katika mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kuendesha shughuli za uvuvi nchini bila ya kuwa na kibali kinyume na sheria za nchi na za Kimataifa. wote walikana mashitaka yao na kurudishwa mahabusu.

kwa Mujibu wa sheria, watuhumiwa hao wakikutwa na hatia watatakiwa kulipa faini ya shilingi bilioni 20, au meli waliyokuwa wanaitumia kufanya uvuvi haramu itataifishwa na kuwa mali ya Tanzania.

Namna ya Kukomesha wezi ktk ATM

Unaweza ukawa umeingia katika ATM machine kwa lengo la kujichukulia vijisenti vya matumizi wiki end hii, lakini ghafla jizi likakufuata na kukulazimisha uchukue fedha. Usibishane nalo maana laweza kukuzuru, unachotakiwa kufanya ni kuingiza namba zako za siri kinyume, kwa mfano namba yako ya siri ni 2009, unachofanya ni kuandika 9002, fedha zitatoka lakini nusu zitakwama kwenye machine na itapiga alam itakayowajulisha polisi bila jizi kujua hadi linakamatwa labda liwe janja likurupuke Mfumo huo umetengenezwa kwa lengo la kutoa msaada endapo kutatokea hatari yoyote.source Feedbitz

Friday, March 13, 2009

Watalii waionyesha kazi Simba

Kama ulidhani walikujakutalii nchini, umekosea timu ya Van couver kutoka Canada jana walionyesha kazi wekundu wa Msimbazi kwa kuwachapa magoli 2-1 katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar, kumbuka Yanga waliwachapa Wacanada hao goli 3-0.

Matajiri wa Dunia

1. William Gates III (53) anaongoza kwa utajiri duniani akiwa na utajiri unaofikia thamani ya dola za Kimarekani bilioni 40, kibopa huyo ni baba wa watoto watatu, ambapo utajiri wake unatokana na microsoft
Kibopa anayemfuatia Bill Gates ni Warren Buffett (78) ambaye ana utajiri unaofikia dola za kimarekani bilioni 37, akiwa ni baba wa watoto watatu ambaye awali alikuwa na mke ambaye alifariki na akaoa mke mwingine, chanzo cha fedha kilichomuwezesha kuwa bilionea ni uwekezaji ndani ya Marekani. Wapo wengi hao ni wawili wa juu
Hao ni wenzetu wakati sie tunabishana juu ya ununuzi wa mitambo ya Dowarns, EPA na wale sijui eti walitumia vubaya ofisi zao na kulisababishia taifa hasara kubwa, wenzetu wanasonga tu, sie twakalia siasa

Thursday, March 12, 2009

Kwa kutuma msg huku hatari inakuja

Kweli Duniani kuna mambo, alianza Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Mnali kwa kuwacharaza bakora walimu wa shule ya Msingi Katerero kwa kile alichodai kuwa hawatimizi majukumu na hata akafikia hatua ya kusema kuwa anajua atafukuzwa kazi, lakini MESSAGE SENT na kweli akafukuzwa kazi. Kabla hatujakaa sawa, Kijana Ibrahim Said nae akamlamba kofi Makamu wa Pili wa Rais Mstaafu na Kipenzi cha watu maarufu kama mzee ruksa naye anadai kuwa alikuwa anatafuta njia ya kufikisha ujumbe kupinga viongozi wa dini kuzungumzia kondomu na ushirikiano baina ya waislamu na wakristo. Soma hapa chini japo ufupi msikie aliyewahi kuwa RPC Mbeya na sasa Dar es Salaam anachozungumza. Kijana anayeshikiliwa kutokana na kumpiga kofi Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitalini kupimwa akili huku Polisi ikiendelea kuchunguza kama anahusika na kikundi chochote cha wanaharakati wenye msimamo mkali. Wakati hatua hiyo ikichukuliwa, taasisi na watu mbalimbali wamelaani kitendo hicho cha kumpiga Rais mstaafu na kusema ni kinyume na maadili ya Watanzania. Kamanda wa Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba kijana huyo, Ibrahim Said (26) aliiambia Polisi kuwa alifanya hivyo kutokana na kuchukizwa na hotuba zinazosisitiza Waislamu kushirikiana na Wakristo. Kova alisema kijana huyo alidai kwamba aliamua kumpiga kiongozi huyo mstaafu kwa sababu hakubaliani na hotuba za viongozi wa Kiislamu zinazosisitiza Waislamu na Wakristo kushirikiana katika kuadhimisha sikukuu za kidini kama vile Maulid, Idd (kwa Waislamu), Pasaka na Krismasi (Wakristo). Kwa mujibu wa Kova, Said alidai kuwa hakuwa na lengo lolote la kumdhuru Rais Mwinyi bali alikuwa akifikisha ujumbe kwa jamii. Kamanda Kova alisema alipohojiwa na Polisi, Said alisema anataka sikukuu za Kiislamu washerehekee kivyao na Wakristo washerehekee peke yao, wasilazimishwe kuwa na umoja. Pia Said alidai anapinga matumizi ya kondomu kwa kuwa watu wakitumia kondomu, watakuwa wamehalalisha uzinifu kwa Waislamu. Kova alisema kutokana na kitendo cha Said kumpiga Rais Mwinyi aliyekuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam juzi saa 12 jioni, alipelekwa jana Muhimbili kabla ya kufikishwa leo mahakamani.

Kutana na Mashabiki wa soka Duniani

Wednesday, March 11, 2009

Heshimaaaaa toa

Ni Vijana wakakamavu, lakini lipo jambo kidogo linasikitisha. Wakiwa kama watanzania wengine wenye ajira, askari wa kampuni binafsi za ulinzi ndio wanaolipwa kiduchu pengine kuliko hata house girl anayefanya kazi kwa kibosile.
Kwanza wanakesha wakilinda mali zenye thamani ya mamilioni ya shilingi, lakini hivi karibuni Chama cha makampuni ya ulinzi binafsi kilitangaza kuwa askari waliopo chini ya makampuni hayo watawajibika kuwalinda albino ili wasiendelee kuawa ingawa bado vitendo hivyo vya kinyama na kishenzi vinaendelea.
Sasa kuna swali huwa najiuliza, hawa walinzi wa sekta binafsi wengi wao mishahara yao ni kati shilingi 25,000 au 35,000 wanafamilia na watu wanaowategemea, kwa kuamua kuwalinda albino ni jambo jema sana,lakini nyie wamiliki hebu waongezeeni mishahara japo kidogo ili wasigeuka kuwa wezi katika maeneo wanayoyalinda.

Tuesday, March 10, 2009

Hongera

Rais Kikwete akimpongeza mwanamke pekee kutoka Afrika Kusini aliyeshiriki katika operesheni ya kuikamata meli ya wavuvi haramu.

Meli hii kuwa mali ya Tanzania?

Askari akilinda meli iliyokamatwa katika bahari ya hindi ikifanya shughuli za uvuvi haramu, hata hivyo meli hiyo haijulikani ni ya nchi gani huku mabaria karibu 30 waliokutwa ndani ya meli hiyo wakishindwa kuhojiwa kwa kile kilichodaiwa kuwa wanazungumza lugha ya ajabu na isiyo eleweka ni ya Taifa gani. ila jana kwenye TV niliwaona kama wakionyesha alama ya dole kwa wapiga picha wa tv.

Habari njema ni kuwa meli hiyo inaweza kuwa mali ya Tanzania ikiwa wamiliki wa meli hiyo watashindwa kulipa faini ya bilioni 20 ikiwa ni kosa la kuingia katika eneo la Tanzania kufanya shughuli za uvuvi haramu bila ya kuwa na vibali.

Yanga Bwana weee acha

Mshambuliaji Ben Mwalala wa Yanga akimtoka beki wa Vancover Whitecaps ya Canada, Trafford mason katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliofanyika uwanja wa Taifa Dar es salaam jana. Katika mchezo huo yanga iliibuka na ushindi mnono wa magoli 3-0, magoli hayo yaliwekwa kimiani na Jerry Tegete aliyepachika mawili na Mkenya Mike Baraza aliyemalizia la tatu.

Kweli Yesu anaweza

Muimbaji wa nyimbo za Injili, Ambele Chapanyota enzi hizo akiwa mmoja wa wakabaji na wezi katika eneo la nonde Jijini.
Baada ya kumpokea Bwana Yesu alibadilika na kuwa mtu mwema katika jamii na ndipo bwana Yesu akamfunulia na kumuonyesha kuwa ana kipaji cha uimbaji na sasa anatamba na Albamu inayokwenda kwa jina 'Salama kwa Yesu' kweli ukimfuata yeye ataukoa, atakubadilisha na kukupa maisha yenye amani duniani.
Akabarikiwa na kupata mke sasa ni mtu mwenye heshima yake, anawasihi vijana waache kutenda maovu kwa kuwa hayampendezi Mungu zaidi ya kuwafanya wawe na maisha ya hofu na kujificha kila wakati, kutengwa na jamii na kuogopwa kama mnyama. Kwake yeye hakuna linaloshindikana na wote tumfuate.

Monday, March 9, 2009

Ona tofauti hii

Tofauti ya tamaduni, ukitembelea visiwa vya Zanzibar ni kawaida kabisa kukutana na wanawake waliojitanda kanga na baibui mwili huku wengine wakiacha macho tu, lakini kwa kuwa visiwa hivyo vimejaliwa kuwa na fukwe nzuri, pia si ajabu kukutana na wanawake wa kizungu wakiwa wamevalia bikini na kanguo kadogo kwa juu kanaitwa sidiria. source Feedblitz

Biashara

Biashara ndogo ndio msingi wa maisha ya watanzania wengi hususani wanawake. ni biashara za machungwa, ndizi, mboga za majani na nyinginezo ambazo hata mtaji wake hauzidi shilingi 50,000,wengi wanaishi katika nyumba za kupanga huku wakiwa na familia zinazowategemea na wanasomesha watoto. Mikopo, Serikali na taasisi za fedha zimekuwa zikiwahamasisha wananchi kukopa ili waweze kuwa na miradi endelevu na inayoweza kuwainua kiuchumi, lakini riba za mikopo hiyo zimekuwa ni tishio na kusababisha wengi washindwe kukopa, pia wengi hawana vitu vya kuwekeza kama dhamana. Ipo haja kwa serikali kuweka mkakati utakaowasaidia watanzania wa kawaida kuwa na uwezo wa kupata mikopo.

Sunday, March 8, 2009

Nyama choma

aaaa kwa jumapili ya leo ukikaa sehemu yenye chama choma huku kukiwa na utulivu wa kutosha na unakamata kinywaji kile Unachopenda maisha yanakuwa matam, picha FeedBlitz