Kupitia blog hii utapata nafasi ya kuyajua mambo yanayojiri kila siku katika Mkoa wa Mbeya zikiwemo, habari mbalimbali zinazohusu jamii, matukio, na tetesi mbalimbali. Pia kupitia blog hii tutajadili masuala mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Mkoa wa Mbeya.
Thursday, February 12, 2009
Breaking news
Kuna taarifa kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ileje na Mkuu wa Kituo cha polisi wilayani humo wanashikiliwa na polisi wa nchini Malawi.
Chanzo; inadaiwa kuwa polisi walikuwa wakiwafuatilia Raia wa Somalia walioingia nchini kinyume cha sheria, hata hivyo wakiwa njiani wakakutana na watu wanavusha bidhaa kwa njia ya magendo na katika harakati za kukabiliana nao polisi walinyang'anywa Bunduki na kisha watu hao wa Magendo kuikabidhi bunduki hiyo kwa polisi wa Kituo cha Chitipa Malawi.
Shughuli ilipoanzia sasa; baada ya kupolwa kwa silaha hiyo, OCD na OSS walikwenda nchini Malawi kwa ajili ya kuchukua bunduki yao, hata hivyo walipofika waliwekwa chini ya ulinzi na hadi muda huu saa 5:56 walikuwa bado hawajaachiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment