Sunday, February 8, 2009

tetesi; barabara ya Mbeya-Chunya

Kuna tetesi kuwa kampuniiliyoshika tenda ya kujenga barabara yenye urefu kilomita 36 kati ya Mbeya-Lwanjiro iliyogharimu fedha za Watanzania shilingi bilioni 27, imeshindwa kuitekeleza kazi hiyo kikamilifu. Ikiwa ni takribani zaidi ya mwaka mmoja na miezi kadhaa sasa, wananchi wanasema kampuni hiyo haina muelekeo wa kuimaliza kazi kwa wakati huku tetesi kutoka ndani ya Kampuni hiyo zikidai kuwa wafanyakazi wamekuwa wakitimuliwa kila kukicha bila sababu za msingi, mafuta kuibwa kwa ushiriki wa baadhi ya viongozi. Kampuni hii pia ina kandarasi nyingine ya kukamilisha ujenzi wa uwanja wa KImataifa wa Songwe. Wenye taarifa zaidi tushirikiane ili tuweze kufahamu uwezo wa kampuni hiyo kiutendaji na kama kazi waliyopewa inawiana na uwezo wao?. kwa kuwa fedha zinazotumika ni za walipa kodi ipo haja kupata ukweli wake.

No comments:

Post a Comment