Saturday, February 28, 2009

Eti malipo ya cheki yanayozidi 10 ml kikomo

Malipo ya cheki zaidi ya milioni kumi kufikia kikomo leo Jamani kuanzi tarehe moja mwezi ujao, mtu yeyote yule ambaye atataka kumlipa mwenzake kiasi cha fedha cha zaidi ya milioni kumi (10,000,000) kwa kutumia cheki ya benki moja ili mlipwaji a-depositi benki nyengine (benki yake), haitawezekana tena. Mfano mwengine ni huu; Yani kama unamdai mtu hela kiasi cha zaidi ya milioni kumi (10,000,000) kisha huyo mtu akulipe kwa kutumia cheki basi wewe kataa maana ukiipeleka hiyo cheki katika benki yako itakataliwa. Lakini kama cheki ni chini ya milioni kumi haina tatizo. Hii ina maana kuwa Clearing House ya Benki Kuu ya Tanzania haikubali malipo binasfi ya cheki zinazo zidi milioni kumi. Badala yake kama unataka kumlipa mtu hela zaidi ya milioni kumi basi njia ni hizi zifuatayo; 1. Mdumbukizie pesa kwenye akaunti yake kwa kuenda wewe binafsi au mwakilishi wako katika benki yake. 2. Nenda katika benki yako kisha uiagize benki yako itume hela kwa mfumo wa TISS (Tanzania Interbank Settlement System) 3. Mlipe taslimu (cash). UFAFANUZI 1. Kama mtu amekupa cheki ya benki ambayo wewe pia una akaunti kwa jina hilo hilo lililoandikwa kwenye Cheki basi haina noma hataka kama imezidi milioni kumi italipwa tu ilimradi mlipaji awe na hela za kutosha kwenye akaunti husika. 2. Malipo yote ya Cheki ya chini ya milioni kumi hatakuwa kama kawaida. 3. Special Clearance ya zaidi ya milioni kumi itakuwa hakuna tena. 4. Malipo yote ya Cheki za Serikali yatakuwa kama kawaida. Ikumbukwe kuwa ni malipo yale tu yanayohusisha benki mbili yani (bank to bank payments) ndio tunayoyaongelea. Source Jamii Forum

Nini sofa! hii ni zaidi ya sofa

Wakati Mijini Mkijidai kwa sofa, sisi pia ni Watanzania na tunafurahia maisha

Friday, February 27, 2009

Breaking News

Nyumba ya Diwani wa Kata ya Tunduma, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Aden Mwakyonde imeshambuliwa kwa kupigwa mawe na kundi la vijana wanaokadiriwa kuwa 50 kwa madai kuwa amewasaliti kwa kukubali operesheni usafi kufanyika katika Mji huo mdogo wa Tunduma ambao ni maarufu kwa biashara. Unapakana na nchi jirani ya Zambia na ni lango la kuingilia nchi za Kusini mwa Afrika. Chanzo chake; Kiukweli mji wa Tunduma umekithiri kwa uchafu na kutokana na hali hiyo Uongozi wa halmashauri hiyo ulitangza operesheni ya siku sita ya kuhakikisha mji unakuwa safi na kufuatia utungaji wa sheria ndogo zitakazosaidia kuhakikisha wananchi wanawajibika kuchangia na kushiriki katika shughuli za usafi. Shughuli ilipoanzia sasa; Kama kawaida operesheni hiyo kama zilivyo nyingi imewahusisha mgambo na askari polisi, na hadi kufikia jana ikiwa ni siku ya nne ya opersheni walikuwa wakikamata watu wanaofanya biashara kando ya barabara, jana wakakamata baiskeli 50 za vijana wanaodaiwa kuvusha mahindi kupeleka nchi jirani ya Zambia. Inadaiwa leo majira ya saa 9 vijana hao wakiwa na mzuka walikwenda kituo cha polisi na kudai warudishiwe baiskeli. hapo sasa zikaibuka Tetesi ambazo zinadaiwa kuwa Mkuu wa Kituo cha polisi cha Tunduma akawaeleza taratibu vijana hao kuwa wao ni watekelezaji wa sheria tu na agizo la kukamata na kufanya usafi limetolewa na Halmashauri ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ni Aden Mwakyonde ambaye pia ndio diwani wa Kata ya Tunduma. Tetesi hizo zinadai kuwa kauli hiyo ya Mkuu wa Kituo ikawapandisha mori vijana hao ambao indaiwa waliondoka wakiwa na hasira hadi nyumbani kwa diwani huyo wakiwa na ghadhabu za aina yake na kuanza kufanya uharibifu mkubwa wa mali kwa kuvunja vioo vya nyumba na inadaiwa walifikia hadi kuvunja masinki ya vyooo aa ajabu kabisa. Nwenyewe Mwakyonde amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, hata hivyo kutokana na uchungu wa kuharibiwa mali zake alishindwa kuzungumza zaidi ikiwa ni kutotaja hasara iliyopatikana au hata kugusia kama kuna mwanafamilia yeyote amejeruhiwa katika kadhia hii. Taarifa zaidi kesho, lakini kuna mambo ya kujiuliza kuhusu kitendo hicho cha vijana ambao tunaweza kuwaita wenye hasira. Tujiulize tu japo kidogo kitendo walichofanya hata kama kweli wangekuwa wameonewa ni sahihi, na je kwanini wamejihalalisha na kuchukua sheria mkononi, Swali kuu kabisa ambalo ni tetesi je kama kweli Mkuu wa Kituo cha Polisi Tunduma alithubutu kutoa kauli hiyo>? huyu kweli ni askari anafaa kuendelea kushikilia nafasi aliyonayo?

Tunatafakari

Mbunge wa Kigoma, Zitto Kabwe akiwa na Mbunge wa Mbarali Estherina Kilasi wakitafakari jambo, wakati wa ziara ya kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za mitaa ilipofanya ziara wilayani Mbozi.

Thursday, February 26, 2009

Watoto na Biashara

Hali ngumu ya maisha inasababisha watoto washirikishwe katika biashara ndogo ndogo, badala ya kutumia muda wao kwa masomo na michezo

Wednesday, February 25, 2009

Ofisi ya Chama cha SAU yawa Grocery

Kuna tetesi kuwa ofisi za Chama cha Sauti ya Umma (SAU) zilizopo Mbalizi wilaya ya Mbeya Vijijini zimegeuzwa kuwa grocery, Tetesi zilizopatikana mitaani zinadai kuwa aliyekuwa mgombea wa chama hicho, Subi Mwakapiki mara baada ya uchaguzi huo ambao uliishia kwa yeye kupata kura zisizozidi wala kufikia kura 500 ndiye mmiliki wa Grocery hiyo. Zipo tetesi zinadai kuwa uongozi wa wilaya wa chama hicho umepanga kumfikisha kwa Pilato mwanamama huyo ambaye alikuwa na ndoto za kuwa mbunge na kuwawakilisha wananchi wa jimbo. kwa ushahidi wa picha fuatilia hapa zaidi

Usalama kwanza

Mkono wa kushoto ni kibao kinachoonyesha kuwa magari hayaruhusiwi kuingia barabara ya kulia na kwamba inaruhusu magari yanayotoka tu.
Dereva wa gari aina ya Rav 4 akivunja sheria kwa makusudi kwa kuingia katika barabara isiyoruhu magari kuingia huku mbele yake kukiwa na gari la kikosi cha usalama barabarani linalotaka kutoka.
Askari wa Kikosi cha usalama barabarani akijaribu kufungua mlango wa gari lililovunja sheria za usalama huku gari lingine likiingia barabarani kwa kufuata sheria.
Askari wa kikosi cha usalama barabarani akiingia kwenye gari tayari kwa kumpeleka kituoni dereva wa gari lililovinja sheria za usalama barabarani

Tuesday, February 24, 2009

Liyumba wa BOT aibuka

Ndugu wadau, yule Liyumba wa Benki Kuu ya Tanzania aliyekuwa amejichimbia katika chimbo lisilojulikana na kuwaweka roho juu Takukuru, leo kaibukia mahakamani na kurejeshwa Rumande baada ya mahakama ya kumuona kuwa si muaminifu. Kumbe bongo nayo kubwa unaweza ukaa uwani tu watu wakakutafuta wakatangaza hadi kutoa mijihela lakini na usikamatwe

Eti polisi kampiga kijana risasi bila sababu?

Kuna tetesi zimeenea kuwa askari polisi mmoja amemjeruhi kijana mmoja mkazi wa mabatini kwa kumpiga risasi ya mguuni kwa kile kinachodaiwa eti ni bahati mbaya. tetesi zaidi zinadai kijana huyo alilazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya na kuruhusiwa kutoka Februari 23, baada ya madaktari kubaini kuwa risasi hiyo ilipita kwenye mnofu na haikugusa mfupa. Kinachosemekana sasa ni kuwa huyo askari aliyemjeruhi kijana huyo alitoa kwa siku mbili tu na kisha akaingia mitini. Wadau fuatilieni ili tupate ukweli wa tetesi hizi kama ni za kweli

Ofisi hii wanaamini Mzee Ruksa bado ni Rais

Mbunge Zitto Kabwe akisisitiza jambo wakati wa ziara ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za mitaa ilipofanya ziara wilayani Mbozi, nyuma ni Picha ya Rais mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi. badala ya kuweka picha ya JK wenzetu hawa sijui wanaishi dunia gani hawatambui kuwa serikali hii ni ya awamu ya nne.
Mbunge wa Mbarali, Estherina Kilasi akizungumza katika kikao hicho naye ni kama hakuiona picha hiyo ya Mwinyi huku ya Mwenyekiti wa CCM na Rais JK ikiwa haipo.
Huyu yeye aliamua kufumba macho kabisa ili asiione
Hadi leo kuna baadhi ya maeneo nchini wanaamini kuwa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu J.K Nyerere ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini kwa walio maofisini yote nchini wanauelewa mpana kwamba Serikali iliyopo Madarakani ya awamu ya nne ikiwa chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Kabla ya Kikwete Marais waliopita ni pamoja na J.K Nyerere, All Hassan Mwinyi, Benjami Mkapa na sasa Rais Kikwete. Kwa taratibu zilizopo ukiingia katika ofisi nyingi hapa nchini, utakuta kuna picha ya Rais wa awamu ya kwanza na aliyepo madarakani kwa wakati.

Monday, February 23, 2009

Gari la kampeni za CCM lateketea

Gari lililoshiriki kampeni za uchaguzi wa Jimbo la Mbeya vijijini likiteketea kwa moto, gari hilo linalomikiwa na studio H. ya Jijini hapa ambalo limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za matangazo ikiwa ni pamoja na ziara za viongozi wa Kitaifa

Ngoma za asili

Utamaduni wa Watanzania

Sunday, February 22, 2009

Hawa nao ni Watanzania

Hawa ni Watanzania waishiyo wilayani Mbarali, kwa shida ya Maji hawatofautiana sana na wenzao wa linaloitwa Jiji la dar es Salaam. Watoto hawa walikutwa wakichota maji katika kisima kilichochimbwa ndani ya mto uliokauka maji.

Saturday, February 21, 2009

Umakini

Zitto Kabwe akiwa na Mkuu wa wiliya ya Mbozi, Halima Kihemba, wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya umma ilipofanya ziara wilayani
humo

Utalii wa ndani

Bongo Camping, moja ya taasisi zinazosaidia kuutangaza utalii wa ndani, Watanzania tunanafasi ya kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini na kuijionea maajabu ya Mwenyezi Mungu badala ya kuwaachia wageni. Tembelea Mbeya uone inavyovutia

Friday, February 20, 2009

Usalama kwanza

Abiria wanashauriwa kutelemka gari linapokuwa katika kituo cha mafuta, lakini abiria wamekuwa wakaidi huku Madereva na Makondakta nao wakishindwa kuwashauri abiria watelemke, hivi kukizuka moto na kusababisha vifo vya abiria, nani wa kulaumiwa? abira, kondakta, dereva au kama kawaida Serikali?

Thursday, February 19, 2009

Liyumba wa BOT ametoroka?

ALIYEKUWA MKUU WA UTUMISHI NA UTAWALA WA BENKI KUU AMATUS JOACHIM LIYUMBA, inasemekana ameingia mitini baada ya kupewa zamana ya kiwango cha chini tofauti na matakwa ya mahakama iliyotaka atoe bilioni 50 ili apate dhamana.
Tetesi zinadai kuwa waliomwekea dhamana mtuhumiwa huyo wa matumizi mabaya ya ofisi wanashikiliwa na polisi huku tetesi zaidi zikidai kuwa pilato aliyemwachia huru kwa dhamana naye yupo msambweni ili ajieleze.Tuwe wavumilivu tukisubiri habari kamili kama

barabara zetu

Licha ya Jiji la Mbeya kubarikiwa kuwa na barabara nyingi za lami, barabara hizo zimegeuka kuwa kero kwa watumiaji wake kutokana na kujaa mashimo na kutofanyiwa ukarabati, kinachotia aibu zaidi ni barabara zinazoingia katika Kituo kikuu cha Mabasi Mbeya, ambapo magari hulazimika kuhama kutoka upande mmoja hadi mwingine na kufanya kuwe na hatari ya kutokea kwa ajali.

Wednesday, February 18, 2009

Mwanafunzi afa akimkimbia

Mwanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya Sekondari ya mchanganyiko ya Mwakaleli wilayani Rungwe, amefariki dunia jana baada ya kujigonga, kupasuka sehemu ya paji la uso wakati walipokuwa wakiwakimbia Walimu. Mwanafunzi huyo Edson Mwanjali (20), alifariki jana alipokuwa akipatiwa matibabu jana katika hospitakli ya Rufaa Mbeya. Chanzo chake.Februari 14 majira ya saa 2 usiku, Mwalimu wa nidhamu wa shule hiyo, John Lazaro (27) akiwa na mwalimu mwenzake Mwete Wilson, waliwa katika ukaguzi wa kawaida wa kukagua nidhamu ya wanafunzi wa shule hiyo ambao ni mchanganyiko wa wavulana na wasichana. Wakiwa wanakatiza katika mitaa ya shule hiyo, ghafla wakaona wanafunzi wakiwa kwenye uwanja wa shule hiyo, na kuamua kwenda kushuhudia ili kuyafanya macho yao yaamini kama ni kweli wameona, lakini wakiwa wanajimuvuzisha, wanafunzi walishitukia mwanga wa kurunzi na kuamua kutimua mbio na hatima Mwanjali kuishia kujigonga katika mwamba wa goli la chuma na hatimaye kufariki kufariki Februari 17. Maswali ya kujiuliza, hawa wanafunzi wamekwenda Sekondari ya mwakaleli kwa ajili ya kusoma, lakini je? uwanjani walikuwa wanafanya nini usiku tena wavulana kwa wasichana. Nao Walimu walikuwa wanatembea tu ama walianza kutimua vumbi ili kukamata japo mwanafunzi mmoja kwa ushahidi. Polisi wanawashikilia walimu hao kupisha uchunguzi na kwa usalama wao maana wanafunzi walirusha mawe kabla ya kuzuiwa na risasi za polisi.

Genius Group

Kundi Jipya la muziki wa kizazi kipya la Genius, linalohaha kutoa albamu yake ya kwanza, tatizo fedha, wadau wasaidieni

Mama na Mtoto

Furaha ya Mama ni kumuona mwanae akiwa na afya njema, apate elimu bora na kufurahi na wenzake, lakini wakina mama wengi wa leo hawawapi fursa watoto yao japo hata kunyonya kidogo na wengine huishia kuwatupa majalalani na kwenye mashimo ya vyoo.

Tuesday, February 17, 2009

Breaking news

Ama kweli ukishangaa ya Musa utayaona ya filauni.Mchungaji wa Kanisa la Pentecoste lililopo Idiwili kata ya Iyula wilayani Mbozi anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kukutwa na mabaki ya mwili binadamu yanayohisiwa kuwa ni mabaki ya mtu mwenye ulemavu wa ngozi (Albino) waliyokuwa wanayauza kwa zaidi ya shilingi milioni 30. Mchungaji huyo, Cosmas Mwasenga (39) anashikiliwa kwa pamoja na Luseshelo Mwashilindi ambaye inadaiwa alikuwa ameyahifadhi nyumbanmi kwake mabaki ya mwili huo, ikiwa ni vipande vinne vikiwamo viwili vinavyosadikiwa kuwa ni sehemu ya mikono ya mabaki ya mwili huo. kweli ipo haja ya kuwachunguza hawa wachungaji wa makanisa ya leo, huyu anaechunga kondoo wa bwana anashiriki kuwapiga deal albino, kinachokera wakati wanatafuta wateja eti wakawa wananadi kuwa wanauza viungo vya kunguru mweupe.

Maisha ya vijana

ni harakati za vijana katika kitafuta kama kijana akiwa katika moja ya mitaa ya Mbeya akitafakari na jinsi ya kukabiliana na Migambo wa Jiji, huku akilazimika kuosha gari lolote linalotekea ili aweze kupata ujira.

Monday, February 16, 2009

Prison wamechoka

Lile jinamizi la kupoteza mechi, limeendelea kuikumba timu ya Tanzania Prison baada ya kuondolewa kwa aibu katika michuano ya kimataifa kwa kuchapwa goli 4 na Walibya na hivyo kufanya jumla ya magoli kuwa 6-0, inawezekana hawa ni Wacomoro waishio Tanzania. Wadau nini kifanyike ili kuikoa timu hii ambayo sasa kati ya mechi tano ilizocheza zikiwemo mbili za Kimataifa imechapwa magoli 13 na yenyewe kutikisa nyavu za wapinzani mara tatu tu"

Unalijua hili

Imebainika kuwa mabinti wengi wanaofanya kazi kwa akina mama wanaopika vyakula katika migahawa midogo ya mitaani maarufu kama mama ntilie, wanatumika pia kama vivutio kwa wateja hasa vijana, wakati wa mama wengine wamewageuza mabinti hao mitaji kwa kuwachagulia hata wanaume wa kwenda kulala nao, hivi na ukimiw huu nini matumaini ya kizazi kijacho. Watoto wengi wanaotumika ni wale wa kati ya miaka 14-20.

Awa Baba akiwa na miaka 13

(Pichani baba na mama wakiwa na mtoto wao).
Ingekuwa ni hapa kwetu Tanzania sijui ingekuwaje, Lakini nchini Uingereza, watoto wawili, Alfie Patten na Chantelle Steadman (15) wamepata mtoto wa kwanza wote wakiwa ni watoto, Hii ni huko Uingereza kumbe ngono za mapema si bongo tu hata kwa wenzetu

Mizaha na Magari

Bila kujali usalama wake, abiria waliokuwa wanasafiri kati ya Kyela kwenda mpaka wa Tanzania na Malawi eneo la Kasumulu akiwa amefungua mlango kuruhusu hewa kuingia ndani bila kujali usalama wa Maisha yake na abiria wengine

Sunday, February 15, 2009

The First family Valentine's Day

The First Family Valentine's Day,
Wakati kwetu siku hii ya wapendao huazimishwa kwa vijana kufanya kufuru ya ngono, unywaji wa pombe kupita kiasi, kutoka na kujimwaga mitaani na nguo za rangi nyekundu, wenzetu ni tofauti kama anavyoonekana President Obama na Mkewe, wao huonyesha mapenzi nyakati zote baina yao. Hivi kwanini kwetu hadi ifike Februari 14, ndipo eti umuonyeshe mwenzi wako kwamba unampenda, tubadilike

watoto na Siasa

Siku za karibuni kumekuwa na ongezeko la watoto wanaohudhuria mikutano ya Kisiasa, wakati idadi ya watoto ikiongezeka idadi ya vijana na watu wazima wanaohudhuria mikutano hiyo inapungua kwa kasi, kunani hapa?

Saturday, February 14, 2009

Mchezo wa Bao

Mchezo wa bao ni maarufu kwa Mikoa ya pwani, huku wachezaji bao pembeni wakiwa na Kahawa, lakini wilayani Kyela mchezo huo huchezwa huku ukihanikizwa na porojo za hapa na pale

Friday, February 13, 2009

Kyela Mitaani

Ukikatiza katika Mitaa ya wilaya ya Kyela, licha ya kushuhudia wingi wa baiskeli lakini pia utakutana na tumbaku inayouzwa mitaani ambayo hupimwa kwa kipimo maarufu kama ndonya

Thursday, February 12, 2009

Nguvu ya Mapenzi

Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa kundi la Victoria, Fabian Kasonya akiwa na kiongozi mwenzake, walipokuwa wakizungumza na Waandishi wa Habari.
Kama ulizoe kuona filamu za wasanii maarufu wa Dar es Salaam, sasa Mbeya nao wameaanza, ni Siku ya Wapendanao Februari 14, Kundi la Victoria Art Group litazindua filamu yake ya kwanza ijulikanyo kama Nguvu ya Mapenzi, fika ukumbi wa Dhandho ushuhudia uzinduzi wa filamu hiyo.

Breaking news

Kuna taarifa kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ileje na Mkuu wa Kituo cha polisi wilayani humo wanashikiliwa na polisi wa nchini Malawi. Chanzo; inadaiwa kuwa polisi walikuwa wakiwafuatilia Raia wa Somalia walioingia nchini kinyume cha sheria, hata hivyo wakiwa njiani wakakutana na watu wanavusha bidhaa kwa njia ya magendo na katika harakati za kukabiliana nao polisi walinyang'anywa Bunduki na kisha watu hao wa Magendo kuikabidhi bunduki hiyo kwa polisi wa Kituo cha Chitipa Malawi. Shughuli ilipoanzia sasa; baada ya kupolwa kwa silaha hiyo, OCD na OSS walikwenda nchini Malawi kwa ajili ya kuchukua bunduki yao, hata hivyo walipofika waliwekwa chini ya ulinzi na hadi muda huu saa 5:56 walikuwa bado hawajaachiwa.

Unaifahamu Noti Nyekundu ya sh 100

Unaifahamu noti Nyekundu ya shilingi 100, ambayo ilitumika miaka ya 70.Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kyela, Japhet Mwakasumi anahadith tofauti kuhusu ugumu wa maisha yeye anasema unasababishwa na mabadiliko ya tabia na utamaduni na wala Serikali haihusiki kabisa na hilo.

Wednesday, February 11, 2009

Usafiri wa baiskeli Kyela

Kama umezoea ukifika sehemu na kukutana na taksi zikiwa zimejipanga kusubiri abiria, hali ni tofauti ukifika wilayani Kyela, usafiri mkubwa wa huko ni baiskeli na unatumika na watu wote wanawake kwa wanaume.

Tuesday, February 10, 2009

Breaking news

Zipo tetesi kuwa watuhumiwa wawili wanaodaiwa kumuua albino Henry Mwakajira aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili wameachiwa huru na mahakama ya wilaya ya Rungwe,siku ya kwanza tu ya kufikishwa mahakamani kwa agizo la Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DDP), nyeti kamili fuatilia zaidi hapa kesho.

Wanafunzi na Matokeo

Wanafunzi waliohitimu kidato cha nne na baadhi ya wazazi wakiwa nje ya Internet ya Posta wakisubiri kutizama matokeo yao. Baadhiyao waliofeli walijikuta wakiangua kilio hadharani

Monday, February 9, 2009

Harakati za kwenda Bungeni

Ni takribani wiki mbili tangu Mchungaji Luckson Mwanjale aingie bungeni kwa kuibuka na kura zaidi ya 32,000 kati ya wapiga kura zaidi ya 120,000. Pichani, Mwanjale akiwa katika harakati za kuvuta gari la Matangazo lililokuwa limekwama wakati wa kampeni zake.
Suala la barabara ni moja ya kero kubwa za Mbeya vijijini, ni takriban miezi 20, atarudi kuomba kura, Mwanjale unakumbuka ahadi zako na adha ulioonja wakati wa harakati zako za kwenda Bungeni?

tetesi mitaani

Zipo tetesi zimeenea kwa takribani siku tano sasa katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mbeya, kuwa Mfanyabiashara mmjoja alimfumania mfanyabiashara mwenzake akiwa na Mkewe. Inadaiwa kuwa mfanyabiashara huyo alikusanya kundi la mabaunsa la baunsa na kumfanyia kitu mbaya mfanyabiashara mwenzake na kumpiga picha. Tetesi zaidi zinadai mfanyabiashara aliefumaniwa alilipishwa shilingi milioni tano ili picha zisisambazwe. Cha Kujiuliza; Wanaume tumekuwa tukichukua uamuzi mkali pindi tunapohisi au kuthibitisha kuwa wake zetu wanatoka nje ya ndoa, Lakini swali la kujiuliza wewe Mwanaume una wanawake wangapi nje ya ndoa yako, mbona mume akifumaniwa na mkewe bado anatema kibezi. naomba michango yenu je ni haki kwa mume kuwa mkali anapofumania ama kufumaniwa?

Sunday, February 8, 2009

tetesi; barabara ya Mbeya-Chunya

Kuna tetesi kuwa kampuniiliyoshika tenda ya kujenga barabara yenye urefu kilomita 36 kati ya Mbeya-Lwanjiro iliyogharimu fedha za Watanzania shilingi bilioni 27, imeshindwa kuitekeleza kazi hiyo kikamilifu. Ikiwa ni takribani zaidi ya mwaka mmoja na miezi kadhaa sasa, wananchi wanasema kampuni hiyo haina muelekeo wa kuimaliza kazi kwa wakati huku tetesi kutoka ndani ya Kampuni hiyo zikidai kuwa wafanyakazi wamekuwa wakitimuliwa kila kukicha bila sababu za msingi, mafuta kuibwa kwa ushiriki wa baadhi ya viongozi. Kampuni hii pia ina kandarasi nyingine ya kukamilisha ujenzi wa uwanja wa KImataifa wa Songwe. Wenye taarifa zaidi tushirikiane ili tuweze kufahamu uwezo wa kampuni hiyo kiutendaji na kama kazi waliyopewa inawiana na uwezo wao?. kwa kuwa fedha zinazotumika ni za walipa kodi ipo haja kupata ukweli wake.

Awilo wa Mbeya

Mwanamuziki anayetamba katika muziki wa asili, maarufu kama Awilo akiwa katika moja ya shughuli zake za muziki na Bendi yake ya Awilo

Saturday, February 7, 2009

watoto na michezo ya hatari

Baadhi ya Watoto katika vijiji vya Galijembe na Igalukwa katika Wilaya ya Mbeya wakicheza michezo ya hatari kwa kupanda miti kuchuma Matunda bila kujali hatari ya kuanguka huku wengine wakipigana mateke.
Michezo ni sehemu muhimu katika maisha ya Mwanadamu, lakini baadhi ya michezo inayofanywa na watoto ni hatari kwa afya na maisha. Wazazi na Walezi ni muhimu kuzingatia na kuwashauri watoto aina ya michezo ambayo si hatari kwa hatari kwa maisha yao.

Friday, February 6, 2009

Prison yaona mwezi

Baada ya kupata vipigo mfululizo, jana timu ya Tanzania Prison iliona Mwezi kwa kuichapa timu ya Mtibwa sugar goli 2-1. Wakati iliwachukua Mtibwa dakika 13 kujipatia goli la kwanza, Prison walilazimika kusubiri hadi dakika ya 75 na 84 pale Laurian Mpalila na Ismail Suleima (zamani akijulina kama Suma Addo) walipoweza kupachika magoli maridadi na kumwacha kipa Shaban Hassan 'Kado' na wenzake wakishika vichwa kwa mshangao. hata hivyo kwa mujibu wa wachambuzi wa soka timu hiyo iliyopteza Mechi nne mfululizo bado ina kazi ya ziada ili iweze kufanya vizuri. Ilianza mzunguko wa pili kwa kuchapwa goli 2-0 na Villa Squard, ikachapwa 3-1 na Simba, ikaburuzwa goli 1-0 na Yanga katika Uwanja wa kumbuklumbu ya Sokoine kabla ya kuchapwa goli 2-0 na Walibya katika Michuano ya Kimataifa. Inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 22.

vijana wakitafuta

Ugumu wa maisha umesababisha vijana watumie mbinu mbalimbali katika kusaka fedha zitkazowawezesha kumudu maisha ya kila siku. Picha ya Juu, baadhi ya wapiga picha wakiwa katika harakati za kupiga picha za katika Uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine, wawahi studio kusafisha na kurudi kuziuza kwa mashabiki wa soka. Picha ya pili, waliokuwa Mawakala wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU) wakiwa nje ya ofisi za Chama hicho zilizopo Mbalizi wakishinikiza walipwe posho ya shilingi 10,000 waliyoahidiwa. Vijana ni moja ya rasimali muhimu kwa Taifa lolote, na ili Taifa liweze kupata maendeleo linahitaji vijana kwa kuwa ndio nguvu kazi ya Taifa. Je Vijana wa Kitanzania wakiwemo wasomi wa vyuo vikuu, wasomi wa kawaida na wale waliopo Mitaani wanatumika ipasavyo, nini kifanyike ili vijana waweze kuwa na maisha bora.

Thursday, February 5, 2009

Prison-ni kweli wanamuhitaji Mwambusi

Pichani: moja ya mashambulizi yaliyoelekezwa langoni kwa Prison katika mchezo uliochezwa katikauwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine na Yanga kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Timu ya Tanzania Prison, katika msimu uliopita ilianza ligi kwa kishindo na kufanikiwa kumaliza ligi ikiwa ya pili na kufanikiwa kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, wakati huo ulikuwa ikinolewa na kocha Juma Mwambusi.
Ikiwa juu ya mafanikio timu hiyo iliamua kuachana na Mwambusi kwa kile kilichodaiwa kutofikia makubaliano ya kimaslahi na kuamua kumkabidhi mikoba mchezaji wa siku nyingi wa timu hiyo James Nestroy na kumrejesha timu Meneja Hassan Mlwilo.
Kilichotokea, tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi kuu ya Vodacom timu hiyo imeshindwa kutamba, katika mzunguko wa pili imepoteza mechi nne mfululizo,tatu za ligi kuu na moja ya Kimataifa. timu hiyo pekee inayowakilisha Mkoa wa Mbeya imepoteza muelekeo na dalili zake si njema.
Tukiwa wadau wa soka je ni kweli pengo la Mwambusi linaonekana katika timu hiyo? au ndio mwanzo wa timu hiyo kuelekea kupotea katika medani ya soka? nani mchawi wa prison, viongozi, makocha au wachezaji wenyewe?

Wednesday, February 4, 2009

Wapiga Debe

Moja ya ajali mbaya za barabarani zilitokea Mkoani Mbeya na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 15
Hapa Mbeya kwa takribani siku nne sasa kuanzia Januari 31, kuna shughuli pevu inaendelea dhidi ya wapiga debe na madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani kwa makusudi.
Hadi kufikia jana wapiga debe zaidi ya 163 wamekamatwa , 143 walifikishwa mahakamani jana na kati ya hao 93 waliachiwa kwa dhamana na wengine 53 kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Lakini hali ikiwa hivyo leseni za madereva 85 wa daraja 'C' ambao wanaamini ni madereva bora kabisa zinashikiliwa na polisi na wanashughuli ya kujaribiwa upya kutokana na kuonekana kuwa ni madereva jeuri na wasiozingatia sheria za usalama barabarani hali inayomtia shaka RPC Zelothe Stephen.
Ndugu zangi hivi ni kweli abiria, wanahitaji kuelekezwa magari ya kupanda wakati hivi sasa mengi yana vibao vinavyoelekeza maeneo mbalimbali wanayotaka kwenda?
Nchi ikiwa imegubikwa na ajali za kutisha zinatokana na madereva wasiojali, Je madereva wanaosababisha ajali kwa makusudi, kwanini wasizuiwe kuendesha magari tena, tunasemaje kuhusu hilo?

wanajeshi, polisi, raia watwangana

juzi Februari 2, majira ya saa 2 usiku katika mji mdogo kulizuka vurugu baina ya Polisi, Wanajeshi na Raia. Chanzo cha vurugu kinadaiwa kuwa ni Askari Polisi kumsimamisha mwendesha Pikipiki ambaye inadaiwa alikuwa hajavaa Helmet na pikipiki ikiwa haina namba. Inadaiwa kuwa katika mahojiano kulitokea kutoelewana na ndipo Mwendesha pikipiki anayedaiwa kuwa ni Mwanajeshi wa kikosi cha Mbalizi alipotaka kuondoka na askari polisi kuiwahi na kuifunga pingu na hatimaye kuzuka vurugu zilizojumuisha makundi matatu, Polisi kwa upande mmoja na Wanajeshi na Wananchi kwa upande mwingine.Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya Zelothe Stephene anasema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa linawahusu askari na litamalizwa kwa taratibu zao. Cha kujiuliza hapa. Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba yeyote anayevunja sheria anapaswa kuchukuliwa hatua kali za kisheria. Ndugu zangu Watanzania tunazungumziaje matukio yanayowahusisha wanajeshi kuvunja sheria kwa makusudi na wakihojiwa ni vurugu mtindo mmoja. Je kuna ukweli kuwa wapo juu ya sheria

Ngoma za Asili

Wakati tukiwa tumeelekeza macho na masikio yetu katika utamaduni wa nchi za kimagharibi kwa kuiga mavazi, utamaduni wao, muziki na hata namna ya kula na kuzungumza na kusahau tamaduni za kwetu hasa katika nyimbo za asili.
Ukifika Mkoani Mbeya hususani katika wilaya ya Mbozi utakumbuka zamani kwa kushuhudia ngoma maridadi za asili na kusahau kabisa mambo ya bongo flava, R&B na miziki ya sebene kutoka kongo na mengineyo huku ukipata vionjo vya asili kuanzia sauti, filimbi hadi midundo ya ngoma.

Vijana

Yesu kweli anaweza, ukimuamini anaweza kubadilisha maisha yako. haya yametokea kwa mwanamuziki Ambele Chapanyota anayetamba na albamu inayokwenda kwa jina la Salama kwa Yesu. kutoka ukibaka hadi kumuimbia bwana. ukiamua unaweza kubadilika na kuachana na maovu