Friday, February 27, 2009

Breaking News

Nyumba ya Diwani wa Kata ya Tunduma, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Aden Mwakyonde imeshambuliwa kwa kupigwa mawe na kundi la vijana wanaokadiriwa kuwa 50 kwa madai kuwa amewasaliti kwa kukubali operesheni usafi kufanyika katika Mji huo mdogo wa Tunduma ambao ni maarufu kwa biashara. Unapakana na nchi jirani ya Zambia na ni lango la kuingilia nchi za Kusini mwa Afrika. Chanzo chake; Kiukweli mji wa Tunduma umekithiri kwa uchafu na kutokana na hali hiyo Uongozi wa halmashauri hiyo ulitangza operesheni ya siku sita ya kuhakikisha mji unakuwa safi na kufuatia utungaji wa sheria ndogo zitakazosaidia kuhakikisha wananchi wanawajibika kuchangia na kushiriki katika shughuli za usafi. Shughuli ilipoanzia sasa; Kama kawaida operesheni hiyo kama zilivyo nyingi imewahusisha mgambo na askari polisi, na hadi kufikia jana ikiwa ni siku ya nne ya opersheni walikuwa wakikamata watu wanaofanya biashara kando ya barabara, jana wakakamata baiskeli 50 za vijana wanaodaiwa kuvusha mahindi kupeleka nchi jirani ya Zambia. Inadaiwa leo majira ya saa 9 vijana hao wakiwa na mzuka walikwenda kituo cha polisi na kudai warudishiwe baiskeli. hapo sasa zikaibuka Tetesi ambazo zinadaiwa kuwa Mkuu wa Kituo cha polisi cha Tunduma akawaeleza taratibu vijana hao kuwa wao ni watekelezaji wa sheria tu na agizo la kukamata na kufanya usafi limetolewa na Halmashauri ambapo Mwenyekiti wa Halmashauri ni Aden Mwakyonde ambaye pia ndio diwani wa Kata ya Tunduma. Tetesi hizo zinadai kuwa kauli hiyo ya Mkuu wa Kituo ikawapandisha mori vijana hao ambao indaiwa waliondoka wakiwa na hasira hadi nyumbani kwa diwani huyo wakiwa na ghadhabu za aina yake na kuanza kufanya uharibifu mkubwa wa mali kwa kuvunja vioo vya nyumba na inadaiwa walifikia hadi kuvunja masinki ya vyooo aa ajabu kabisa. Nwenyewe Mwakyonde amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, hata hivyo kutokana na uchungu wa kuharibiwa mali zake alishindwa kuzungumza zaidi ikiwa ni kutotaja hasara iliyopatikana au hata kugusia kama kuna mwanafamilia yeyote amejeruhiwa katika kadhia hii. Taarifa zaidi kesho, lakini kuna mambo ya kujiuliza kuhusu kitendo hicho cha vijana ambao tunaweza kuwaita wenye hasira. Tujiulize tu japo kidogo kitendo walichofanya hata kama kweli wangekuwa wameonewa ni sahihi, na je kwanini wamejihalalisha na kuchukua sheria mkononi, Swali kuu kabisa ambalo ni tetesi je kama kweli Mkuu wa Kituo cha Polisi Tunduma alithubutu kutoa kauli hiyo>? huyu kweli ni askari anafaa kuendelea kushikilia nafasi aliyonayo?

No comments:

Post a Comment