
Muimbaji wa nyimbo za Injili, Ambele Chapanyota enzi hizo akiwa mmoja wa wakabaji na wezi katika eneo la nonde Jijini.

Baada ya kumpokea Bwana Yesu alibadilika na kuwa mtu mwema katika jamii na ndipo bwana Yesu akamfunulia na kumuonyesha kuwa ana kipaji cha uimbaji na sasa anatamba na Albamu inayokwenda kwa jina 'Salama kwa Yesu' kweli ukimfuata yeye ataukoa, atakubadilisha na kukupa maisha yenye amani duniani.

Akabarikiwa na kupata mke sasa ni mtu mwenye heshima yake, anawasihi vijana waache kutenda maovu kwa kuwa hayampendezi Mungu zaidi ya kuwafanya wawe na maisha ya hofu na kujificha kila wakati, kutengwa na jamii na kuogopwa kama mnyama. Kwake yeye hakuna linaloshindikana na wote tumfuate.
Ama kweli watu wanabadilika, afadhali kawa kijana mzuri na naona ana mke mzuri, ila kijana ana pozi za kishua.
ReplyDeleteMama
put it in English and we will also be able to read this
ReplyDelete