Kupitia blog hii utapata nafasi ya kuyajua mambo yanayojiri kila siku katika Mkoa wa Mbeya zikiwemo, habari mbalimbali zinazohusu jamii, matukio, na tetesi mbalimbali. Pia kupitia blog hii tutajadili masuala mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Mkoa wa Mbeya.
Wednesday, March 4, 2009
Ujambazi wa kutumia silaha waibuka tena Mbeya
Wale majambazi waliokuwa wanatamba na kufanya unyang'anyi wa kutumia silaha wameibuka tena.
Kundi la Watu 10 wanaodhaniwa kuwa majambazi wakiwa wamebeba silaha na nondo juzi usiku walivamia kiwanda cha nguo (Mbeya Textile) kilichopo Songwe wilaya ya Mbeya na kuiba sefu ya kuhifadhia fedha, kuwajeruhi walinzi watatu, kuwapora bunduki tatu ikiwamo shortgun moja na kukimbilia kusikojulikana.
Majambazi hao wanaoonekana wababe wakiwa na silaha na nondo, walivamia kiwanda hicho majira ya saa 8 usiku na kuwaweka chini ya ulinzi, walinzi watatu waliokuwa wamebeba bunduki tatu, mbili rifle na shortgun moja.
Kwa habari kamili kesho
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment