Sunday, March 8, 2009

Ajali, Llori lagonga kipanya na kuua 4, 17 hoi

WATU wanne wamekufa wakiwemo watatu waliokufa papo hapo na wengine 17 kujeruhiwa vibaya baada ya basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace walilokuwa wakisafiria kutoka Tukuyu kuja Mbeya Mjini kugongwa kwa nyuma na lori la mizigo. Ajali hiyo ilitokea juzi majira ya saa 1:55 usiku katika barabara ya Tukuyu-Mbeya ambapo alisema kuwa ajali hiyo ilihusisha magari matatu. Waliokufa katika ajali hiyo ambao wote walikuwa kwenye basi dogo la abiria kuwa ni pamoja na kondakta wa Toyota Hiace Martin Daimon, Daud Mwaigwiso, mtoto mdogo mwenye umri wa miaka miwili, James Msesa, na msichana mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20-25 ambaye hajatambuliwa . Waliojeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kuwa ni Eli Samson (7), Zainab Sege (45), Eda Kibinga (38), Angesisye Mbilinyi (32) wote wakazi wa kijiji cha Ntokela wilayani Rungwe. Wengine waliojeruhiwa katika ajali hiyo ni Upendo Rashind (28), Deltha Mbogela (35),Telesia John (38), Hassan Ally (39), Elizabert Elia (31), Haruna Fungo (45), Elia Msenye (28), Ashel Mbilinyi (40), Hilda Kasewa (13) na Fatuma Kapusi, Tedy Msesa na Osca Kasewa Ajali yenyewe ilikuwa hivi, basi dogo la abiria lenye namba usajili T 568 AAE liligongwa kwa nyuma na lori la mizigo namba T 499 AJA likiwa na tela lake T 476 AJA aina ya Volvo, likiendeshwa na Ally Mohamed, lilikuwa limebeba karanga kutokea nchini Malawi kuelekea Uyole likiendeshwa . Kabla ya kuigonga kwa nyuma Toyota Hiace,Lori hilo lilianza kuligonga lori jingine la mafuta lenye namba za usajili T 283 ARE na tela lake no. T 668 ARA mali ya kampuni ya Dhandhoo lililokuwa likipeleka mafuta nchini Malawi. Hawa madereva wanafanya mzaha na roho zetu, tusiwaache watatumaliza Mwisho.

No comments:

Post a Comment