Friday, March 6, 2009

Wanafunzi nusura wamacharaze bakora Mkuu wao wa shule

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nzondahaki iliyopo katika Kata ya Nzovwe Jijini Mbeya, Ritha Mtweve juzi alinusurika kupigwa viboko na wanafunzi wa shule hiyo, kwa madai kuwa amekuwa akiwatolea lugha chafu pamoja na kutowasomea taarifa ya miradi ya elimu ya kujitegema. Katika vurugu hizo, wanafunzi hao wa kidato cha kwanza hadi cha tatu waliokuwa wamebeba mawe na fimbo walivunja madirisha kwa mawe, kuwajeruhi walimu wawili pamoja na kuwacharaza bakora wanafunzi wenzao waliogoma kushiriki katika vurugu hizo. Wanafunzi hao waliokuwa wamejaa mchecheto, huku wakishangilia na kupiga makelele wakiwa wamebeba mawe na bakora waliwaamuru walimu wengine warudi majumbani kwao na wamuache mkuu wa shule hiyo hali ambayo iliwatia hofu walimu na kuamua wote kubaki na kujifungia ofisini Kitendo cha walimu wengine kugoma kuondoka kiliwapandisha jazba na kuanza kurusha mawe ambapo waliwajeruhi walimu wawili. Hii ni inakumbusha katika shule ya Katerero Mkoani Kagera ambapo walimu walikuwa bakora kwa amri ya dc, lakini hawa wanafunzi walitaka wamchampe mkuu wa wao kwa lugha chafu, kutosoma taarifa na ukosefu wa vitabu

No comments:

Post a Comment