Kupitia blog hii utapata nafasi ya kuyajua mambo yanayojiri kila siku katika Mkoa wa Mbeya zikiwemo, habari mbalimbali zinazohusu jamii, matukio, na tetesi mbalimbali. Pia kupitia blog hii tutajadili masuala mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Mkoa wa Mbeya.
Tuesday, March 3, 2009
Rais, Mkuu wa Majeshi Guinea wauawa
Askari waasi wamemuua kwa risasi Rais Joao Bernardo Vieira, maofisa wa serikali wamesema. Habari hizo zilikuja jana saa chache baada ya mauaji ya mkuu wa majeshi ambaye alikuwa katika mtafaruku na Rais.
Milio ya risasi ilisikika jijini hapa na mpaka leo hakukuwa na taarifa za nani anaiongoza serikali. Nchi hii ni moja ya nchi masikini sana duniani, na ina historia ya mapinduzi ya serikali na imekuwa njia kuu ya dawa za kulevya, hususan kokeni kwenda Ulaya. Taarifa ziliwakariri maofisa wa kijeshi na serikali waliosema Rais ameuawa.
"Rais Vieira aliuawa na Jeshi alipokuwa akijaribu kukimbia makazi yake ambayo yalishambuliwa na kikundi cha wanajeshi watiifu kwa aliyekuwa Mkuu wa Majeshi Tagme Na Waie, mapema asubuhi hii," msemaji wa Jeshi, Zamora Induta aliiambia AFP.
Alimtuhumu Rais Vieira kwa kuhusika na mauaji ya mkuu wa majeshi. Jenerali Tagme aliuawa baada ya mlipuko kusikika juzi na kuharibu sehemu ya makao makuu ya jeshi. Msaidizi wake, Luteni Kanali Bwam Nhamtchio, alisema Tagme alikuwa ofisini mlipuko huo ulipotokea.
"Alijeruhiwa sana asingeweza kupona. Hili ni pigo kwetu sote," alisema Nhamtchio. Takriban watu watano waliripotiwa kuuawa na mlipuko huo. Kutokana na mashambulizi hayo dhidi ya makao makuu ya Jeshi, maofisa waliviamuru vituo viwili vya redio kusitisha matangazo.
"Kwa usalama wenu waandishi wa habari, fungeni kituo na kuacha kutangaza. Ni kwa usalama wenu," msemaji wa Jeshi Samuel Fernandes aliwaambia waandishi wa habari katika moja ya vituo hivyo. "Tunakwenda kupambana na wavamizi na kujilinda," aliongeza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment