Saturday, March 7, 2009

Wanaume kuhamishiwa Mimba

Mwene Mkuu wa Wasafwa wa wilaya ya Mbeya, Shao Soja Masoko akiwa na mkuu wa Mkoa wa Mbeya, John Mwakipesile wakati wa mkutano baina ya kiongozi huyo na wazee wa mila.
Mwakipesile akiagana na Chifu Mwashinga mara baada ya mkutano huo na chini ni baadhi ya machifu waliohudhuria mkutano huo, Sasa kama ulikuwa hujui kama mwanaume anaweza kupata mimba, soma hapa chini
Kwa wale wanaume wakwale, ambao hawapendi kuona sketi na vijisuruali vya mabinti hasa wanafunzi wakatize hivi, hadi wawatoe nguo katika guest na magetho kiama chao kinakuja.Wazee wa Mila wa kabila la wasafwa, wameiomba Serikali Mkoani Mbeya iwape kibali ili waweze kuwashughulikia wanaume wanaowapa mimba wanafunzi na kusababisha wakatize masomo huku wao wakidunda mitaani na kuwaacha mabinti hao na vitumbo bila msaada.
Mwene Mkuu, Masoko, alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kuwa wao wanakamati zao za ufundi na kama serikali ikiwapa kibali watawashughulikia wanaume wanaowajaza mimba wanafunzi kwa kuwahamishia katika matumbo yao na wanafunzi kuendelea na masomo kama kawaida, "yaani ipo hivi wewe, kwa mfano Juma umejifanya kidume unampa mimba Vanesa ambaye ni mwanafunzi, sasa hawa machifu kupitia darubini zao wanakuona wewe ndio muhusika, na kwa kutumia kamati ya ufundi wanachukua hiyo mimba na kuiweka katika tumbo lako'
Lakini wazee wa mila hao wakasonga mbele zaidi na kusema wapiga nondo nao wakae tayari tayari kwa kuwa kupitia darubini zao watawaona na kuwatengua miguu, kuwafanya wajipeleke polisi na walio na viungo vya binadamu watajitokeza hadharani wakiwa wamevibeba na polisi kuwakamata kiulaini kama wananawa. Habri ndio hiyo tukae mkao wa kula tukisubiri kuona wanaume wakiwa na mimba na si vitambi tena.

No comments:

Post a Comment