Wednesday, December 11, 2013

Michezo


 Hatimaye baada ya hadithi za muda mrefu na shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kuufungia uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine Mbeya, iwanja huo umeanza kufanyiwa ukarabati katika eneo la kuchezea (pitch) ili uweze kuwa kwenye kiwango na kuweza kutumika kwa michuano mbalimbali ya mpira wa miguu.

Meneja wa Uwanja huo, Modestus Mwaluka anasema tatizo la uwanja huo sio kubwa sana na ukarabati wake utakuwa ni wa muda mfupi na uwanja utakuwa tayari kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya vodacom.

 Picha ya juu na chini zikionyesha ukarabati unaoendelea katika uwanja huo ambao unatumiwa na timu ya Tanzania Prisons na Mbeya City kama uwanja wa nyumbani. Mara kadhaa uwanja huo umekuwa ukilalamikiwa hasa na timu za Yanga na Simba kuwa ni mbovu na haufai hasa katika nyakati ambazo zinashindwa kuibuka na ushindi na zikishinda uwanja huwa unakuwa ni mzuri.


Hata hivyo pamoja na ukarabati wa sehemu ya kuchezea bado wamiliki wa uwanja huo wanakabiliwa na changamoto ya kuhakikisha uwanja huo unakuwa katika hali ya usafi na kuboresha mazingira katika nyakati zote ikiwemo kujenga vyoo vipya kwa ajili ya mashabiki wa soka na wananchi wanaofika uwanjani hapo kwa shughuli mbalimbali.

No comments:

Post a Comment