Zaidi ya Baiskeli
100 zenye thamani ya shilingi milioni 16.5 zimegawiwa kwa wakulima wa kahawa,
wahamasishaji wa kilimo hifadhi pamoja na wakulima wawezeshaji katika
wilaya nne za Mkoa wa Mbeya zinazijihusisha na kilimo cha kahawa.
Meneja shughuli
wa shirika la Hanns R. Neumann Stiftung Africa Ltd, Webster Miyanda alisema
lengo la kugawa baiskeli hizo ni kuwawezesha wakulima na wahamasishaji wa
kilimo hifadhi kuweza kutekeleza majukumu yao ya kila siku ambapo
wakulima waliofadika ni wa wilaya za Mbeya, Ileje, Rungwe na Mbozi.
Alisema wameamua
kugawa baiskeli hizo kwa wakulima kwa kuwa wamebaini zinarahisha shughuli kwa
wakulima ambapo alisema hivi sasa wamehasika kuhudhuria mafunzo ya kilimo
bora cha kahawa, ufuatiliaji wa mabadiliko ya tabia nchi kwa kuchukua jotoridi
la kila siku na uboreshaji na uendelezaji wa kilimo hifadhi cha mahindi.
“Hii ni awamu ya
pili, awali tulitoa baiskeli 100 na baada ya kuona kuwa kunamatokeo chanya kwa
wakulima na wawezeshaji wa kilimo hifadhi tumeona tuongeze zingine na lengo
letu ni kuhakikisha wakulima wote wanapata baiskeli ili waweze kufika kwenye
mikutano yao ya vijiji na kushiriki mafunzo kwa urahisi” alisema.
Aidha Miyanda
alisema kabla ya kugawa baiskeli, wakulima walikuwa hawatekelezi miradi na
mafunzo wanayokuwa wamepewa, “kwa mfano tulikuwa tunaandaa shamba darasa na
kuwafundisha, tukiondoka hadi tunarudi hakuna linalokuwa limefanyika, hivyo
tukagundua kwamba usafiri ni tatizo katika utekelezaji na tukaona tuanze kwa
kuwapa baiskeli” alisema.
Kadhalika alisema
upatikanaji wa baiskeli hizo umerahisha wahamasishaji na wawezeshaji kuweza
kushirikiana kwa urahisi na kuweza kubadilishana taarifa na maafisa ugani hivyo
kusaidia kuboresha shughuli za kilimo hivyo kumsaidia mkulima kuboresha kipato
chake.
Kwa upande wake,
muhamasishaji wa kilimo cha kahawa kutoka kijiji cha Igale, alisema kukosekana
kwa mvua za uhakika kumeanza kuathiri shughuli za kilimo cha kahawa, ambapo
alisema kuwa ili kukabiliana na tatizo hulo hivi sasa wameanza kuweka matandazo
mashambani ili kuhifadhi unyevu unyevu kwenye miche ya kahawa.
Akizungumzia
msaada wa baiskeli, alisema zimewasaidia katika kuharakisha utendaji wa
shughuli za kila siku ambapo hivi sasa wanaweza kusafiri kutoka eneo moja hadi
jingine bila ya kulazimika kutembea kwa mguu kama ilivyokuwa zamani jambo
ambalo lilikuwa linakwamisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Shirika la Hanns
R. Neumann Stiftunga Africa Ltf limekuwa likijihusha na utoaji wa elimu ya
kilimo bora cha kahawa pamoja na kuwawezesha wakulima kukabiliana na mabadiliko
ya tabia nchi ambayo kwa kiasi kikubwa yanaathiri kilimo cha zao hilo.
No comments:
Post a Comment