Dodoma kupitia Mtera kwenda Mbeya
*Safari ya jasho, mateso na vilio kwa watoto.
Njia
iliyozoeleka kwa wasafiri wanaotoka Mkoa wa Mbeya kwenda Makao Makuu ya nchi
Mkoani Dodoma ni kupitia Mikoa Iringa, Morogoro na hatimaye Dodoma ambapo safari ni takribani zaidi ya masaa 14
barabarani kwa maana unaondoka Mbeya saa 12 asubuhi na kufika Dodoma kati ya
saa 1 na saa 2 usiku.
Kilichojiri sasa
Safari
ilianza saa 12:00 asubuhi kama ilivyoandikwa kwenye tiketi, lakini baada ya
hapo gari lilianza kupakia kila abiria waliokuwepo barabarani na kusababisha
hali ya hewa ndani ya basi kubadilika na kuwa ya joto kali, vilio kwa watoto na
mateso kwa abiria waliosimama na waliokaa huku wakiwa hawana hata nafasi ya
kusimama wala kusogea.
Miundombinu
ya barabara ni mizuri na kwa kiwango kikubwa barabara ni ya rami.Ipo haja kwa
wamiliki wa vyombo vya usafirishaji abiria kuongeza magari katika barabara hiyo
ili kuwasaidia wananchi wa maeneo hayo waweze kusafiri kwa usalama na amani
tofauti na sasa ambapo usafiri ni wa mashaka
na unaofanya abiria kujiuliza je tutafika na roho zetu?
Abiria wakiwa wameminyana ndani ya basi kiasi cha kusababisha vilio kwa watoto kutokana na joto kal;i, kukosekana kwa hewa ya kutosha.(picha zote na Merali Chawe
Usafiri huu wa basi, na idadi kubwa ya abiria
waliojazana na kusababisha watu kukosa hewa safi,kuvuja jasho mithili ya mtu
aliyetoka kuoga, ukanikumbusha wafungwa waliokufa wilayani Mbarali kutokana
kukosa hewa.
Licha ya kukosa hewa wasafiri wanakuwa katika hatari
kubwa ya kupata magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa kama kifua kikuu,
kikohozi na mangine ambayo kwa njia moja ama nyingine yanasababisha waathirika
kushindwa kushiriki katika shughuli za kiuchumi
Dodoma kwenda Mbeya kupitia Mtera ni njia nzuri na fupi
wamiliki wa magari ya biashara pelekeni magari yenu, lakini yawe yenye kiwango
na sio mabovu.
No comments:
Post a Comment