Kupitia blog hii utapata nafasi ya kuyajua mambo yanayojiri kila siku katika Mkoa wa Mbeya zikiwemo, habari mbalimbali zinazohusu jamii, matukio, na tetesi mbalimbali. Pia kupitia blog hii tutajadili masuala mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Mkoa wa Mbeya.
Saturday, January 24, 2009
siasa
Baada ya siku 28 za kampeni, kesho wananhi wa Jimbo la Mbeya Vijijini watahimisha shughuli hiyo kwa kumchagua Mbunge wao, ambaye wanaamini sera zake zinaweza kutatua kero zao za msingi ikiwamo tatizo la maji.
Lakini wakati kesho ni siku ya kupiga kura yapo baadhi ya matatizo yalijitokeza ikiwamo vyama kushutumiana kuwa kila kimoja kinanunua shahada za wapiga kura, matusi dhidi ya wagombea na vurugu za bendera za CCM na CUF kudaiwa kuchanwa na kutumbukizwa kwenye tope, kubwa zaidi ni kuwepo madai kuwa Chadema inawashinikiza wananchi wasijitokeze kupiga kura
Jimbo la Mbeya vijijini lina kata 17 na wakazi zaidi ya laki 3, lakini waliojiandkisha kupiga kura ni takribani wakazi 120,000, fuatana nami ili kujua je wapiga wameitikia mwito wa Msajili wa vyama aliyewataka kupuuza wanaowashawishi wasipige kura, ikiwa wananchi watakaopiga kura hawatafika nusu ya waliojiandikisha je kutakuwa na mshindi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment