Saturday, January 31, 2009

vijana

Vijana wa CCM wakijivinjari katika Mitaa ya Jiji la Mbeya wakisubiri kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Mbeya Vijijini

Wednesday, January 28, 2009

Wananchi kususia uchaguzi Mbeya, kunani?

Picha ya Juu: Makamu Mwenyekiti Mstaafu, John Malecela akimnadi mchungaji Mwanjale
wakati wa kampeni
Picha ya Chini: Aliyekuwa mgombea wa Chadema, Mwanasheria Sambwee Shitambala, wa pili
kulia akiwa na mashabiki wa Chadema waliomsindikiza kurudisha na hatimaye
kuenguliwa
Januari 25, wananchi wa jimbo la Mbeya Vijijini walipiga kura kwa ajili ya kumchagua mbunge wao atakayemrithi aliyekuwa mbunge wa Jimbo hilo Richard Nyaulawa aliyefariki Novemba 9, mwaka jana kwa ugonjwa wa saratani ya utumbo.
Mchungaji wa Kanisa la Uinjilisti, Luckson Mwanjale ndiye aliyefanikiwa kuibuka kidedea na kumbwaga vibaya mgombea wa CUF, Daud Mponzi ambaye kitaaluma na Mhandisi na Mwanamama mfanyabiashara Subi Mwakipiki. Lakini ushindi huo wa CCM umeachwa maswali zaidi kuliko fura.
Waliojiandikisha kupiga kura walikuwa ni Watanzania 127,780, waliopiga kura ni 44,855 wananchi 82,925 hawakupiga kura hali ambayo inadaiwa kusababishwa Chadema kuenguliwa katika uchaguzi huo na ukosefu wa elimu ya demokrasia.
Watanzania wenzangu, tunamaoni gani katika hili.

Tuesday, January 27, 2009

barabara

Nilibahatika kuzunguka katika jimbo la Mbeya Vijijini wakati wa kampeni za uchaguzi, swali nilijiuliza hivi hawa wanasiasa wanapoombakura na kupotea kwa miaka mitano, wanatahamini maisha ya wananchi wa kawaida.
Mbali ya matatizo ya umeme, maji na barabara, yapo maeneo watoto kwa watu wazima wanavaa nguo ambazo mijini wengine mnapigia deki au kuchoma moto kwa uchakavu mdogo tu.

Vijana

Ili uchumi wa Taifa lolote uweze kukua kwa kasi inahitajika nguvu kazi ya vijana ambayo ikiwa ikitumiwa kwa usahihi inaweza kuleta mabadiliko na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi wa nchi kwa kupitia sekta rasmi na isiyo rasmi.
Lakini kwa Tanzania, licha ya kuwa na rasimali nyingi pamoja na vijana wenye nguvu, ukosefu wa mitaji, vijana kutowezeshwa wengi wameishia kuwa wamachinga, kutembea na soksi mbili siku nzima akitafuta wateja na wengine kuishia kujiajiri kwa kuuza ndizi za kuchoma. Je watawala wetu wanania ya dhati ya kuwakomboa vijana?

Saturday, January 24, 2009

CUF Wakijinadi

Mgombea wa Chama Cha Wananchi (CUF), Daud Mponzi akijinadi wakati wa kampeni za uchaguzi wa jimbo la Mbeya vijijini zilizofikia tamati leo.

Kampeni Za CCM

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbeya, Willium Simwali maarufu kama simwali akicheza ngoma ya asili katika moja ya kampeni za CCM.

siasa

Baada ya siku 28 za kampeni, kesho wananhi wa Jimbo la Mbeya Vijijini watahimisha shughuli hiyo kwa kumchagua Mbunge wao, ambaye wanaamini sera zake zinaweza kutatua kero zao za msingi ikiwamo tatizo la maji. Lakini wakati kesho ni siku ya kupiga kura yapo baadhi ya matatizo yalijitokeza ikiwamo vyama kushutumiana kuwa kila kimoja kinanunua shahada za wapiga kura, matusi dhidi ya wagombea na vurugu za bendera za CCM na CUF kudaiwa kuchanwa na kutumbukizwa kwenye tope, kubwa zaidi ni kuwepo madai kuwa Chadema inawashinikiza wananchi wasijitokeze kupiga kura Jimbo la Mbeya vijijini lina kata 17 na wakazi zaidi ya laki 3, lakini waliojiandkisha kupiga kura ni takribani wakazi 120,000, fuatana nami ili kujua je wapiga wameitikia mwito wa Msajili wa vyama aliyewataka kupuuza wanaowashawishi wasipige kura, ikiwa wananchi watakaopiga kura hawatafika nusu ya waliojiandikisha je kutakuwa na mshindi.