Wednesday, October 27, 2010

Pweza Paul

Pweza Paul afariki

Pweza Paul aliyeondokea kuwa mtabiri maarufu katika michuano ya Kombe la dunia 2010, amefariki. Paul amefariki kifo cha kawaida, ambapo kwa mujibu wa wataalam, Pweza huishi kwa wastani wa miaka miwili na nusu na Pweza Paul alikuwa tayari katika umri umri

Tuesday, October 19, 2010

Siasa

Ni kama anasema 'tatizo lenu hamnielewi nyie waandishi sijasema hilo, oo nasinzia kwa msisitizo

Monday, October 18, 2010

Siasa

Nani anasema eti tunabebwa na malori kwenda kwenye kampeni?sie tunasafari zetu kwani kuvaa sare imekuwa kosa?ndivyo wanavyoelekea kusema

Thursday, October 14, 2010

Mama na mtoto

Aaaa nimeyaona magimbi ngoja nimuwahi anayeuza hata mososi wa hapa restaurant siutaki tena, ni kama anavyoelekea kusema kijana anayetoka restaurant. magimbi kwa chai usipime

Wednesday, October 13, 2010

Vijana

Haa unadhani ntakusaidia, najifanya niko busy naangalia pembeni, nani kakwambia uzidishe mzigo"ni kama anasema mpitanjia.

Tuesday, October 12, 2010

Uwindaji

aaaa maisha ya vijijini kwetu raha mustarehe, hakuna haja ya kupanga foleni kwenye butcher, aa sie twawinda ndege enzi hizo tunaita vinjuni, huku kwetu lakini sijui kijijini kwenu, "aaa simkosi huyo lazima nimdungue"

Monday, October 11, 2010

Kwa taarifa yako

Enzi hizo, nakumbuka sarakasi tulikuwa tunaangalia mashuleni wakija wanne star na wenzake, sie tulikuwa tukimwita wane, lakini kwa sasa mchezo huo si maarufu ingawa si maarufu.

Mitaani kwetu

Mchezo wenyewe ulianza hivi, aisee mi ntakutoa ngeu hivi hunifahamu eee?????
Haa yaani tumevua mashati nakukimbia lakini bado unakuja?hivi unadhani sikuogopi nitakutoa meno ohoo
aaaaa nyie mtauana achanen, mnajifanya wajanja wee muachie mwenzako utamuua.
Kama Kenya wengine wanatazama sinema ya bure tena masumbwi kavu kavu ambayo ni adimu huku wengine wakisonga na shughuli zao kama kawa.