Saturday, May 22, 2010

Hawa nao ni watoto wa Kitanzania

Hawa nao ni watoto wa Kitanzania waliopo Iganjo uyole Jijini Mbeya, watoto hawa nao wapo Tanzania na ni watanzania, hapa walikuwa wametoka kuogelea katika mto na kukutana na baadhi ya waandishi waliokuwa wametembelea mradi wa umwagiliaji wa Iganjo.
Mwandishi wa Baraka FM ya Jiji Mbeya akizungumza na mmoja wa watoto huku mwenzake akifanyajitihada za kuhakikisha suruali yake isimdondoke.Uwezeshaji kiuchumi wananchi utasaidia kuboresha maisha sawa kwa watoto wote na wao kuweza kumudu kusoma katika shule bora,kuishi maisha bora kama ilivyo kwa watoto wengine.

3 comments:

  1. Chawe mbona hao watoto wanaonekana wana afya nzuri tuu tena wanafurahia maisha kama kuogelea huo ndio utaratibu wa Uyole, funikafunika hizo nyeti za bwana mdogo kama kaka mtu anavyojitahidi jamani picha imenifurahisha sana wengi wetu tulianza hivyo hakuna ajabu yoyote

    ReplyDelete
  2. HII PICHA NIMEIPENDA SANA IPO MWAKE SANA INANIKUMBUSHA KALE KULE TULIKOTOKA

    ReplyDelete
  3. Hii picha nimeipenda pia. Imenikumbusha utoto wangu, maana nami nilikulia kijijini, na tulikuwa tunacheza hivi hivi, tunachunga mbuzi na ng'ombe, na tunawinda ndege, panzi, na kadhalika huko porini. Tulikuwa tunakimbia hivi hivi bila viatu, na wakati mwingi tulikuwa na vumbi mwili mzima, hadi jioni, tulipokuwa tunaswagwa na mama au bibi kwenda kuoga.

    Watafiti sasa wanasema kuwa maisha yetu haya, ya kukumbana na vumbi utotoni na ungaunga wa maua na majani huko porini, ni njia ya kujenga kinga mwilini dhidi ya maambukizi ya magonjwa.

    Watafiti wanasema kuwa mambo haya ya siku hizi ya kuwatunza watoto ndani nyumbani, bila hata chembe ya vumbi, na kuwaaacha wanaangalia runinga tu (yaani TV) yanawasabishia madhara kiafya, kama vile kuwakosesha hii kinga niliyosemea hapo juu.

    Kwa hivi, tuwe makini tunaposhangilia hayo tunayoita maisha ya kisasa au maendeleo.

    ReplyDelete