Saturday, May 22, 2010

Hawa nao ni watoto wa Kitanzania

Hawa nao ni watoto wa Kitanzania waliopo Iganjo uyole Jijini Mbeya, watoto hawa nao wapo Tanzania na ni watanzania, hapa walikuwa wametoka kuogelea katika mto na kukutana na baadhi ya waandishi waliokuwa wametembelea mradi wa umwagiliaji wa Iganjo.
Mwandishi wa Baraka FM ya Jiji Mbeya akizungumza na mmoja wa watoto huku mwenzake akifanyajitihada za kuhakikisha suruali yake isimdondoke.Uwezeshaji kiuchumi wananchi utasaidia kuboresha maisha sawa kwa watoto wote na wao kuweza kumudu kusoma katika shule bora,kuishi maisha bora kama ilivyo kwa watoto wengine.

Friday, May 21, 2010

Tutapona kweli

Wakulima wa Bonde la Uyole wakisafisha karoti katika mto ulio karibu na daraja la Igawilo nje kidogo ya Jiji la Mbeya.Baadhi ya watu wanatabia ya kula karoti zikiwa hazijaoshwa mara baada tu ya kununua kutoka sokoni. Ofisi ya Mkemia Mkuu imefunguliwa Mbeya ni nafasi ya ofisi hiyo kuchunguza kama maji hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu.

Thursday, May 20, 2010

Kilimo Kwanza na waandishi

Wakulima wa Iganjo wakiwa wanapanda viazi.Uyole ni moja ya eneo linaloongoza kwa uzalishaji wa viazi,nyanya, vitunguu na mahindi, ambapo eneo hilo linategemea zaidi kilimo cha umwagiliaji.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa wanamuhoji mmoja wa wakulima katika mashamba ya umwagiliaji ya Iganjo.

Wednesday, May 19, 2010

Ofisi ya Mkemia Mkuu sasa Nyanda za Juu Kusini

Kwa wale wenye tabia ya kupachika mimba wanafunzi, wanaokataa au kusingiziwa watoto, kubaini wanaohusika na mauaji ya watoto na uchunaji ngozi pamoja na uchunguzi wa kisayansi kama kwa maji ya kisima na mengine. Sawa dawa ipo sebuleni na si jikoni tena Baada ya Mkemia Mkuu kufungua ofisi kwa Mikoa ya Nyanda za Juu kusini. Wananchi tutumie fursa hii kwa ajili ya utatuzi wa mambo mbalimbali yanahusiana na tafiti za kisayansi.Tuelewe kuwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali si kwa ajili ya kushughulikia masuala ya jinai tu

Monday, May 17, 2010

Siku ya familia Duniani

Jumamosi, May 15, nilibahatika kuhudhuria maadhimisho ya siku ya familia Duniani ambayo Jijini Mbeya yaliazimishwa katika viwanja vya shule ya msingi Nzovwe, kwa umuhimu wa siku yenyewe iliyoandaliwa na taasisi ya Champion nilitaraji wazazi wangehudhuria kwa wingi, lakini idadi ya watoto ilikuwa kubwa huku matumizi ya kondomu yakihimizwa
Picha ya juu ni baadhi ya vijana walioshiriki katika maadhimisho ya siku hiyo wakiwa na kondomu za familia walizogawiwa, na chini baadhi ya watoto waliokuwa wamejazana katika uwanja huo