
Kupitia blog hii utapata nafasi ya kuyajua mambo yanayojiri kila siku katika Mkoa wa Mbeya zikiwemo, habari mbalimbali zinazohusu jamii, matukio, na tetesi mbalimbali. Pia kupitia blog hii tutajadili masuala mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Mkoa wa Mbeya.
Sunday, March 21, 2010
Mmmh Miss wetu

Saturday, March 20, 2010
usafiri wetu
Saturday, March 6, 2010
Mama na Mtoto

Mtoto Xavier King (pichani) aliwaacha watu vinywa wazi baada ya kuanza kutembea bila kutambaa tofauti na hatua za ukuaji wa kawaida wa mtoto.
Mtoto huyo ambaye Februari 15, mwaka huu alitimiza miezi sita, alinyanyuka ghafla wiki moja kabla ya siku hiyo na kutembea akiwa ameshika ukuta. Hiyo ilikuwa hatua yake ya kwanza ya kuanza kutembea bila msaada wowote. Hatua hiyo haikuwashangaza sana wazazi wake, kwani waliamini kwamba alikuwa akicheza, ikizingatiwa kuwa mara kwa mara alikuwa akianguka. Siku mbili baadaye, mtoto huyo alianza kutembea bila kushika popote., mara hiyo akifanya hivyo kwa umbali wa futi sita kutoka mahali anapokuwa. Hapo ndipo alipowashangaza wazazi wake. “Sikuwa na mawazo hayo na kamwe sikuwahi kufikiria jambo la ajabu la aina hiyo. Kama mzazi niliishia kushangaa, nilimpigia simu baba yake kazini na kumwabia, naye alishangaa, “ anasema mama wa mtoto huyo, Mary King (30).
Mzazi huyo ambaye ni muuguzi anasema, watoto wengi huweza kutembea baada ya kufikisha miezi 10 ama mwaka mmoja.
Subscribe to:
Posts (Atom)