Desemba 27 kipyenga cha kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Mbeya vijijini kitaanza vumbi kwa Wagombea wa Vyama vya CCM, Chadema, CUF na SAU kuanza kujinadi ili waweze kupata ridhaa ya wananchi ili waweze kuongoza.
Kinyang'anyiro kikubwa zaidi kinatarajiwa kuwa kwa Vyma vya CCM na Chadema huku Chadema ikionekana zaidi kwa kufanya dodoso la chini kwa chini kabla ya kuamua kusimamisha mgombea wake ambaye ni Mwanasheria Kitaaluma na mstaafu wa JWTZ, Sambwee Shitambala.
Kinatarajia kujiri katika kampeni za uchaguzi huo utakaofanyika Januari 25, ni tuhuma za ufisadi kama silaha pekee inayotegemewa na Chadema kama njia ya kwenda katika Jumba la kisasa kule Dodoma huku CCM ikiwa imemsimamisha mgombea anayeonekana kutokubalika miongoni mwa wanaccm ikiwa imeanza kujihami kwa kumtaka Mbowe naye ajieleze kuhusu tuhuma za ufisadi zinazomkabili.
Mengi yatasemwa lakini kwa wananchi wa Jimbo la Mbeya Vijijini wanayomatatizo ya msingi ambayo ni lazima wawahoji hawa wagombea ni kwa vipi watasaidia kuyatatua hususani suala la miundombinu ya barabara, maji na umeme.
Wananchi wa Mbeya Vijijini wanatakiwa kutumia akili za kuambiwa na wasiasa mahili wa kujieleza, lakini nadhani ipo haja kwa wananchi hao kutumia akili za kuambia, wakazichuja na kuchanga na akili zao ili waone kipi ni mchele na kipi pumba.
Kwa uchache tunatarajia kampeni zinazohanikizwa na miungurumo ya Helkpota ya Chadema huku CCM wakigwaya kuleta ya kwao kwa kisingizio cha gharama ingawa kiukweli wanaohofu kuwakuta ya tarime huku wakiwa wamemwaga mijihela.
Tchao.